Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mzee Nyerere alivyofanyiwa mwaka 1983 na wakina Hans Poppe na Maganga alikuwa siyo Mwenyekiti wa Chama ???
Au unadhania kwamba Babu wetu mpendwa aling'atukwa Ikulu kwa amani tu ??? Mzee Karume alipeleka hadi Majasusi (Viwavi Jeshi) Ujerumani Mashariki lakini nini kilimtokea mwishoni ??? Hichi ndicho Watawala wetu wanakosea sana, kuhisi hawawezi kuguswa kwasababu wamepewa madaraka makubwa. Mimi simuombei vibaya Raisi wangu kabisa na ninapenda sana afanikiwe kwa kila jambo lake. Japo nikiangalia huu mwenendo wake naona kabisa atatumbukia kwenye shimo kubwa sana la giza, maana katika kusoma kwangu kote Historia ya dunia tokea mwaka 1814 kipindi cha Von Matternich hadi kufika mwaka 1989 kipindi cha Nicolae Ceausescu hakuna mtawala mwenye hulka kama za Raisi Magufuli aliyefanikiwa kuongoza nchi bila kukumbwa na balaa la Kisiasa au Uchumi. Hayupo, Hayupo, Hayupo....!
.
 
Na huu ndiyo umasikini mkubwa wa Watanzania wengi: Kukubali nchi ya zaidi ya watu Milioni 50 kuongozwa kwa matakwa ya mtu moja tu kwa msaada wa genge lake. Haiwezekani Raisi akawa na nguvu bila kuwa na chombo maalumu cha kumzuia asijifanyie anayotaka kila uchwao: Raisi anavunja miiko ya Kikatiba, Utawala wa Sheria na kuvuruga uchumi wa nchi wa halafu hakuna hata mtu mkweli na muwazi anayemkemea, unategemea tutafika kwa mwendo huu kweli ??? Kila mtu anakwambia mwache Raisi alete maendeleo kwasababu tumechelewa. Sasa sijui hata kama dhana ya Maendeleo kama wanaielewa au wanadhani kuwa na Electric Trains, Sky-Scrappers na Airfields ndiyo maendeleo. Kuna mdau moja humu aliwahi kusema kwamba Watanzaia siyo Masikini bali ni Wajinga sana.....Ujinga ndiyo adui namba moja wa Mtanzania...

NB: Success is a formula, and we can just predict it by simply looking at steps you follow.
Waliofuata kanuni siku zote walifanikiwa na waliopuuza kanuni walishindwa vibaya sana kama Mzee Nyerere!
Hapa kwenye ujinga ni tatizo kubwa mno, yaani kirusi cha ujinga ni zaidi ya Ebola
 
Maeneo ya katikati ya Jiji la Mwanza leo Mei 11, 2018 yatakosa umeme kwa saa nane baada ya transfoma na nyaya za umeme kuanguka eneo la Kauma na kuziba barabara ya stesheni.



Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zinaeleza kuwa nishati hiyo itarejea kuanzia saa 11 jioni.



Akizungumza na MCL Digital leo ofisa uhusiano wa Tanesco jijini Mwanza, Flaviana Moshi amesema nguzo hizo zimedondoka saa 2 asubuhi na kuathiri upatikanaji wa umeme kwa maeneo mengi ya jiji hilo.



Mmoja wa mashuhudia, Jamali Dauda amesema wakati akiendelea na shughuli zake ameshuhudia nguzo zikianguka na bahati nzuri eneo zilipoangukia hakukua na mtu yeyote
 
Siku moja baada ya msanii Steve Nyerere, kudaiwa kutafuna michango ya msiba wa video Qeen, Agnes Masogange, dada yake Emmy Gerald amesema msimamo wake hautofautiani na kamati ya mazishi inayosimamiwa na msanii huyo ya kumfungulia mtoto akaunti kama ilivyopangwa hapo awali.

Akizungumza na MCL Digital leo Mei 11, Emmy amesema siku mbili hizi anatarajia kuwapa taarifa kamili za mtoto huyo ili waweze kumwekea hela yake kama ilivyopangwa.
 
Jamani naomba watu wapuuze maneno yanayosemwa kuhusu hiyo michango, mimi naungana na kamati ya mazishi kumfungulia mtoto akaunti na nitawapa taarifa zake kamili kwa ajili kuanza mchakato wa kuifungua, kwani tayari nimeshapata ujumbe wao wa kulitaka hilo,” amesema dada huyo.

Hata hivyo, amesema kwa huyo aliyeenda kulalamika kwenye vyombo vya habari ni ndugu wa mwanaume aliyezaa na Masogange na kueleza jambo lolote linalohusu hayo aulizwe yeye kwa kuwa ndio msemaji wa familia upande wa kina Masogange.
 
Alipoulizwa kama wana mahusiano mazuri na upande wa baba wa mtoto, alisema hawana tatizo lolote na kueleza kwamba hivi karibuni wanatarajia kuwa na kikao cha wana ndugu kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo arobaini yake.
 
Unajua haya mambo kwa sasa sitaki kuyaongea sana kwenye vyombo vya habari, kwani kuzungumza ni sawa na kumsengenya marehemu ambaye ana siku chache tangu tulivyompumzisha, nitaongea mengi siku ya arobaini ikiwemo kuwashukuru watu walivyoshiriki katika msiba wake hayo mambo mengine naomba watu wayapuuze,” amesema Emmy.
 
Jana mweka hazina wa kamati ya mazishi ya Masogange, Zamaradi Mketema alisema Sh2.1 milioni zilizobaki katika mazishi anazo yeye na anachosubiri ni kupata taarifa kamili za mtoto ili waweze kumfungulia akaunti hiyo.

Masongane alifariki Aprili 20, mwaka huu, akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mama Ngoma, na kuzikwa Aprili 23 kijijini kwa baba yake Utengule Mbeya.
 
Klabu ya Manchester City imemuaga kwa heshima ya aina yake mchezaji nguli, Yaya Toure kwenye Uwanja wa Etihad.

Nahodha huyo wa zamani wa Ivory Coast, jana alicheza mchezo wa mwisho kwenye uwanja huo baada ya kudumu kwa miaka minane.

Katika mchezo wa jana usiku, Yaya alikuwa nahodha na aliingoza Man City kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton.
 
Nguli huyo mwenye miaka 34, ametangaza kuondoka Man City baada ya mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi mwishoni mwa msimu.

Wachezaji wa Man City na Brighton walipanga mstari na Yaya kumuaga na muda mfupi baadaye nahodha Vincent Kompany alimtaja nguli huyo ni shujaa wa Man City.

“Unastahili kuagwa kwa heshima kubwa kama hii, wewe ni gwiji wa Man City na utabaki kuwa shujaa wa Man City,”alisema Kompany.
 
Nguli huyo mwenye miaka 34, ametangaza kuondoka Man City baada ya mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi mwishoni mwa msimu.

Wachezaji wa Man City na Brighton walipanga mstari na Yaya kumuaga na muda mfupi baadaye nahodha Vincent Kompany alimtaja nguli huyo ni shujaa wa Man City.

“Unastahili kuagwa kwa heshima kubwa kama hii, wewe ni gwiji wa Man City na utabaki kuwa shujaa wa Man City,”alisema Kompany.
 
Yaya alikabidhiwa picha huku kaka yake Kolo Toure aliyewahi kucheza Man City akishuhudia pembeni.

Uwanja wa Etihad ilipambwa na mabango yenye picha za kiungo huyo na baadhi ya mashabiki wakiwemo watoto walimpamba kwa majina tofauti.

Hata baada ya kutoka wachezaji wenzake walimkumbatia huku Sadio Sane akionyesha hisia kwa nguli huyo walipokuwa wamekumbatiana. Yaya alitoka dakika tano kabla ya mpira kumalizika na alikwenda moja kwa moja kumkumbatia kocha Pep Guardiola.
 
Siasa za CCM na CHADEMA huwa zinanichekeshaga sana, yaani uenyekiti ni Umungu mtu. Inabidi tubadilike bwana na tukumbuke kwamba tunajenga nyumba moja na hakuna mtu wa maana sana kuliko mwenzake.
Siyo CCM na CHADEMA peke yake. Ni vyama vyote. Rafiki yangu Mh. John Momose Cheyo na UDP yake tangu enzi zile mpaka imemfia mikononi. Mh. Mrema na TLP na kwingine alikopita...Bado...
 
Back
Top Bottom