Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

852901457_29265.jpg
 
Mkuu wakati mwingine unatamani uwe ulikosea kusema huyu jamaa ni janga la Taifa lakini kwenye ukweli uongo hujitenga. Waliosema huyu jamaa ni janga la Taifa ndani ya hii miaka miwili wako 100% accurate. Katiba inadharauliwa, mahakama na Bunge vyote vinadharauliwa, sheria za nchi zinapindishwa vile atakavyo yeye. Watanzania wanatekwa, wanateswa, wanauwawa Serikali kimyaaaa hakuna uchunguzi wala baba yake uchunguzi!

Hazina trillions zinachotwa bila idhini ya Bunge, CAG anadharauliwa kaandika kuhusu upotevu wa 1.5 trillions badala ya kuunda Tume kuchunguza kulikoni hoja yake nzito inapotezewa kaandika kuhusu Serikali kulipa zaidi ya bilioni 200 kwa madeni hewa Serikali imedharau. Naendelea kusema ni janga la Taifa tena kubwa sana huyu hatuhitaji kusubiri 2020 kutoa tathmini hii miaka miwili na nusu inatosha kabisa.

Ila jamaa anaharibu nchi aisee.
 
Back
Top Bottom