MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Siasa za CCM na CHADEMA huwa zinanichekeshaga sana, yaani uenyekiti ni Umungu mtu. Inabidi tubadilike bwana na tukumbuke kwamba tunajenga nyumba moja na hakuna mtu wa maana sana kuliko mwenzake.Kwani macheameni wa vyama vyetu vya siasa huwa hawaguswi?
.Mzee Nyerere alivyofanyiwa mwaka 1983 na wakina Hans Poppe na Maganga alikuwa siyo Mwenyekiti wa Chama ???
Au unadhania kwamba Babu wetu mpendwa aling'atukwa Ikulu kwa amani tu ??? Mzee Karume alipeleka hadi Majasusi (Viwavi Jeshi) Ujerumani Mashariki lakini nini kilimtokea mwishoni ??? Hichi ndicho Watawala wetu wanakosea sana, kuhisi hawawezi kuguswa kwasababu wamepewa madaraka makubwa. Mimi simuombei vibaya Raisi wangu kabisa na ninapenda sana afanikiwe kwa kila jambo lake. Japo nikiangalia huu mwenendo wake naona kabisa atatumbukia kwenye shimo kubwa sana la giza, maana katika kusoma kwangu kote Historia ya dunia tokea mwaka 1814 kipindi cha Von Matternich hadi kufika mwaka 1989 kipindi cha Nicolae Ceausescu hakuna mtawala mwenye hulka kama za Raisi Magufuli aliyefanikiwa kuongoza nchi bila kukumbwa na balaa la Kisiasa au Uchumi. Hayupo, Hayupo, Hayupo....!
Hapa kwenye ujinga ni tatizo kubwa mno, yaani kirusi cha ujinga ni zaidi ya EbolaNa huu ndiyo umasikini mkubwa wa Watanzania wengi: Kukubali nchi ya zaidi ya watu Milioni 50 kuongozwa kwa matakwa ya mtu moja tu kwa msaada wa genge lake. Haiwezekani Raisi akawa na nguvu bila kuwa na chombo maalumu cha kumzuia asijifanyie anayotaka kila uchwao: Raisi anavunja miiko ya Kikatiba, Utawala wa Sheria na kuvuruga uchumi wa nchi wa halafu hakuna hata mtu mkweli na muwazi anayemkemea, unategemea tutafika kwa mwendo huu kweli ??? Kila mtu anakwambia mwache Raisi alete maendeleo kwasababu tumechelewa. Sasa sijui hata kama dhana ya Maendeleo kama wanaielewa au wanadhani kuwa na Electric Trains, Sky-Scrappers na Airfields ndiyo maendeleo. Kuna mdau moja humu aliwahi kusema kwamba Watanzaia siyo Masikini bali ni Wajinga sana.....Ujinga ndiyo adui namba moja wa Mtanzania...
NB: Success is a formula, and we can just predict it by simply looking at steps you follow.
Waliofuata kanuni siku zote walifanikiwa na waliopuuza kanuni walishindwa vibaya sana kama Mzee Nyerere!
Wahenga waliwahi kusema:Hapa kwenye ujinga ni tatizo kubwa mno, yaani kirusi cha ujinga ni zaidi ya Ebola
Siyo CCM na CHADEMA peke yake. Ni vyama vyote. Rafiki yangu Mh. John Momose Cheyo na UDP yake tangu enzi zile mpaka imemfia mikononi. Mh. Mrema na TLP na kwingine alikopita...Bado...Siasa za CCM na CHADEMA huwa zinanichekeshaga sana, yaani uenyekiti ni Umungu mtu. Inabidi tubadilike bwana na tukumbuke kwamba tunajenga nyumba moja na hakuna mtu wa maana sana kuliko mwenzake.