Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hizi Ndizo Faida Utakazozipata Kutokana Na kupumzika

MUUNGWANA BLOG / 19 hours ago



Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, watu wengi hawapati muda wa kutosha wa kupumzika. Mara nyingi mtu anapozidiwa hupunguza zaidi muda wa kupumzika ili akamilishe majukumu yake.

Ni wazi kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kupumzika, ndiyo maana hawatengi muda wa kutosha wa kupumzika. Ni ukweli usiopingika kuwa kupumzika kuna manufaa makubwa sana kwenye miili na utendaji wetu wa kazi kila siku.

Ikiwa unataka kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida za kupumzika.

1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu
Ubongo wa mwanadamu, unahitaji kupumzika ili uweze kujijenga na kufanya kazi vyema. Ikiwa mtu hatapata muda wa kutosha wa kupumzika, uwezo wake wa kutunza kumbukumbu utapungua.

Pia utafiti uliofanyika umebaini kuwa kutokupumzika huongeza kiasi fulani cha protini kwenye ubongo ambacho huchangia katika kutokea kwa maradhi ya Alzheimer (Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu).

2. Huondoa hatari ya kupata kiharusi
Kiharusi ni ugonjwa unaosababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo ya damu kwenye ubongo; hili husababisha damu kuvuja ndani ya ubongo.

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa uchovu hasa ule unaoambatana na msongo wa mawazo, unaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo na kisha kusababisha ugonjwa wa kiharusi.

3. Hulinda afya ya moyo
Kupumzika kuna manufaa makubwa kwenye afya ya moyo wako. Ni wazi kuwa kasi ya usukumaji wa damu wakati wa kufanya shughuli mbalimbali ni tofauti na wakati unapokuwa umepumzika.

Hivyo basi, unapopata muda wa kupumzika unaupa moyo wako nafasi ya kupunguziwa mzigo wa kusukuma damu kwa kasi, ambao umeubeba wakati ulipokuwa unafanya shughuli mbalimbali.

4. Hutoa muda wa mwili kujijenga
Miili yetu inahitaji kujijenga kila mara hasa baada ya shughuli nyingi. Kwa njia ya kupumzika utaweza kuupa mwili wako nafasi nzuri ya kujijenga na kurejeshha tena nguvu iliyotumika wakati wa shughuli mbalimbali.

5. Huongeza hamasa ya utendaji
Nani anapenda kufanya kazi akiwa amechoka? Naamini hakuna. Kupata muda wa kutosha wa kupumzika kutakuwezesha kujisikia vizuri na kuwa tayari kutekeleza majukumu yaliyoko mbele yako.

Ikiwa basi unataka kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, ni muhimu kuhakikisha unapata muda wa kutosha wa kupumzika.


6. Huimarisha misuli
Tunapopumzika misuli yetu inajijenga na kurudisha ute wake uliopotea wakati wa shughuli mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kila baada ya kazi tunapata muda wa kutosha wa kupumzika ili tuboreshe afya za miili yetu.


7. Huimarisha kinga mwili
Kinga mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga mwili kujijenga na kujiimarisha.

8. Huondoa msongo wa mawazo
Chanzo kimojawapo cha msongo wa mawazo ni uchovu, na chanzo kimojawapo cha maradhi mbalimbali ni msongo wa mawazo.

Hivyo ni muhimu kuhakikisha tunapumzika ili akili na fikra zetu zijisafi na kutuepusha na tatizo la msongo wa mawazo.
 
Utafiti: Wanawake wa Rwanda na Kenya ndio wataishi muda mrefu zaidi Afrika Mashariki

MUUNGWANA BLOG / 7 hours ago




Wanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu.

Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0.

Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5.

Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini.

Kwa wanaume, umri wa kuishi ulikuwa miaka 62.6 kufikia mwaka 2016 ukilinganisha na miaka 53.7 mwaka 1990. Kwa kiwango cha kadiri, umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kwa miaka kumi kufikia sasa tangu mwaka 1990.

Nchini Kenya, umri wa kuishi kwa wanawake umeongezeka kutoka miaka 62.6 mwaka 1990 hadi miaka 69 mwaka 2016, ongezeko la takriban miaka sita, lakini kwa wanaume ongezeko limekuwa ni kutoka miaka 60.2 hadi miaka 64.7, miaka 4.5.

Nchini Uganda, umri wa kuishi kwa wanawake sasa ni miaka 64.7 (sawa na umri wa wanaume kuishi Kenya) na kwa wanaume ni miaka 59.8.

Kiwango hicho hata hivyo kimeimarika kwa zaidi ya miaka 10 kwa kila jinsia kwani mwaka 1990 umri wa wanawake kuishi Uganda ulikuwa miaka 52.1 na kwa wanaume 46.3.

Kwa sasa, kwa kawaida, kila mwanamke aliyefikisha umri wa kujaliwa mtoto nchini humo huwapata watoto 4.7 ukilinganisha na watoto 3.7 kwa kila mwanamke Mkenya.

Pato la jumla kwa kila raia Tanzania kufikia mwaka jana lilikuwa $2,516 lakini Kenya lilikuwa $2,925, tofauti ikiwa $409.

Uganda, ambapo pato kwa kila raia kila mwaka ni $1,838, kila mwanamke hujifungua watoto 5.6.
 
Wanawake waandamana Nairobi

MUUNGWANA BLOG / 1 hour ago




Wanawake Nchini Kenya wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za kufukuzwa kwa mwanamke mmoja katika mgahawa mmoja kwa kumyonyesha mtoto wake.

Wanawake hao wameelekea katika mgahawa wa Olive Restaurant, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye mri wa mwaka mmoja.

Taarifa hiyo imezusha hisia za watu wengi nchini humo na kusababisha makundi ya kutetea haki za wanawake kuandaa maandamano.

Wakina mama hao wamesema maandamano ya leo ni kushinikiza haki za akina mama waungwe mkono na kusaidiwa katika kufanikisha kuwanyonyesha watoto wao bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
 
Wewe unaweka habari nzima nzima. Numbisa anakata kata tuvipande tudogo tudogoooooo...Safi sana. Tuelimisheni na kutuhabarisha tu...
 
Mohandas Karamchand Gandhi(Kigujarati: મોહનદાસ કરમચંદ ગાંધી:2 Oktoba 1869 -30 Januari 1948), maarufu zaidi kwa jina la Mahatma Gandhi, alikuwamwanasheria, mwanafalsafa, mpiganaji wahaki za binadamu na kiongozi wa siasa nchiniUhindi.
Anajulikana hasa kama kiongozi wa harakati za uhuru wa Uhindi aliyepinga na kushindaukoloni kwa njia ya amani bila ya matumizi wa mabavu au silaha.
 
Maisha
Gandhi alizaliwa katika eneo laGujarat kama mtoto mdogo wa Karamchand Gandhi na mama Putali Bai. Baba yake alikuwa waziri mkuu katika serikali yamaharaja wa nchi lindwa ndogo ya Porbandarwakati ilipokuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza.
Familia yake ilifuata dini ya Uhindumadhehebu ya Wavishnu lakini nyumba ya Gandhi ilitembelewa pia na Waislamu naWajain.
Mwaka 1883 akiwa na umri wa miaka 13 aliozwa kwa mke wake Kasturba wakazaa watoto 4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…