Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Falsafa ya Satyagraha
Katika miaka híyo Gandhi alijenga falsafa yake ya upinzani bila ya silaha wala mabavu aliyotumia baadaye Uhindi.
Imani ya Ghandi iliathiriwa na mafundisho yaUjain aliyojua tangu utoto wake na hasa dai la kutotumia mabavu lakini kufuata njia za amani.
 
Kiini chake kilikuwa satyagrahainayomaanisha "kusimama upande wa ukweli". Satyagraha kwake ilikuja pamoja na kutokuwa na uhasama na kutotumia nguvu. Alisema "Ukweli haukubali nguvu kwa sababu hakuna mtu mwenye ukweli wote, kwa hiyo hakuna mwenye haki ya kuadhibu wengine."
 
Dhana nyingine ni "swaraj" inayomaanisha "kujitawala". Gandhi aliona swaraj kwa ngazi mbili:
swaraj kama kujitawala kwa kila mtu akitawala tamaa zake;swaraj kama haki ya watu kwa pamoja kujiamulia mambo yao na kutotawaliwa na nje (kwa mfano na wakoloni).
 
Kiongozi Uhindi
Baada ya kuugua aliondoka Afrika Kusini 1914 akarudi Uhindi alipopokewa kama shujaa kwa sababu habari zake zilimtangulia.
Aliunda makazi ya pamoja (ashram) alimoishi pamoja na watu waliofuata imani yake ya satyagraha. Alianza kuvaa nguo za wakulima wa kawaida.
 
Mwaka 1920 alikuwa kiongozi wa Indian National Congress akaanzisha kampeni ya kitaifa dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza. Alihimiza Wahindi wengi kutotii sheria za serikali ya Kiingereza bila kutumia nguvu.
 
Mfano moja ni maandamano ya chumvimwaka 1930. Sheria ya Kiingereza iliwekabiashara yote ya chumvi mikononi mwa serikali. Kutengeneza chumvi na kuiuza ilikuwa haki ya serikali iliyokabidhi haki hii kwa makampuni waliolipa kodi za pekee. Gandhi aliongoza watu maelfu baharini walipochota maji ya bahari wakaichemsha na kupata chumvi kidogo kwa njia hiyo. Kiasi cha chumvi kilikuwa kidogo mno, lakini kwa kufanya hivyo walivunja sheria kwa kusudi. Waingereza walianza kuwakamata wapikachumv
 
lakini walishindwa na idadi kubwa ya watu waliokubali kukamatwa. Tena ilikuwa vigumu kuwahamasisha askari walioona kosa lilikuwa dogo sana na wakosaji hawakuwa hatari yoyote kwao.
Gandhi mwenyewe alikamatwa mara kadhaa akakaa jela jumla ya miaka 8.
 
tapatalk_1526393737309.jpeg
 
Ahsante.
Wamuache mama wa marehemu anung'unike, maumivu anayo pitia ni makali sana. Ingekuwa Sitivini yupo hai na ana kesi ya kubinjuka na katoto kakubwa,hilo lingekuwa lake. Angepambana na hali yake
Na kabint kalikua mcharuko mno na mahakaman alisema alikua na uhusiano ma marehemu kwa miez mitano sijui mitatu,mwaka huo huo wa ajali alisherehekea birthday akisema kafikisha miaka 20 means alibanjuka na marehem akiwa na 19yrs

Wanaomlaum mama kanumba wajiulize mbona wao wanailaumu serikali kumuachia askar aliyeua mwanafunz ndan ya daladala,je akifungwa askar mwanafunz atarud au?

Lulu angeacha janja janja akamaliza kifungo chake kwa amani,hii kitu itamtesa sana
 
Kipindi cha uhuru na ugawaji wa Uhindi
Ndani ya Uhindi wenyewe fitina ilianza juu ya nafasi ya Waislamu katika taifa jipya, huku sehemu kubwa ya Waislamu wakidai kugawiwa kwa koloni katika nchi mbili.
Mapigano yalianza na watu maelfu waliuawa. Mnamo Agosti 1947 nchi mbili za Uhindi naPakistan zilianzishwa, na Oktoba 1947 vitavikafuata kati ya nchi zote mbili juu ya jimbo la Kashmir. Vita vikaongeza uadui, na watu mamilioni walifukuzwa yaani Wahindu kutoka Pakistan na Waislamu kutoka Uhindi.
Gandhi alijitahidi kupatanisha viongozi wa pande zote akafunga chakula akitangaza alikuwa tayari kufunga hadi kifo wasipopatana. Heshima kwa Gandhi ilisababisha viongozi wa pande mbalimbali katika Uhindi kukutana na kutafuta njia za kumaliza uhasama.
 
Kifo
Tarehe 30 Januari 1948 Gandhi alipigwa risasi na kuuawa akitembea katika bustani ya nyumba huko Delhi. Mwuaji wake alikuwa Mhindu wa kundi lililofuata itikadi kali. Huyu kijana alikasirishwa na hatua za kupatanisha Waislamu na Wahindu akaamini Gandhi alikuwa msaliti wa Uhindu.
Mahatma
Gandhi alijulikana hasa kwa jina la Mahatma. Neno hili la Kisanskrit lamaanisha "roho kubwa". Aliitwa hivyo mara ya kwanza alipofika Bombay wakati wa kurudi kutoka Afrika Kusini. Gandhi hakupenda jina hilo lakini alishindwa kuzuia matumizi yake.
 
Back
Top Bottom