Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa Ujerumani Joachim Low aikimbia Arsenal

MUUNGWANA BLOG / 32 minutes ago




Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low ameongeza mkataba wake wa kuendelea kuifundisha timu hiyo mpaka ifikapo 2022.

Rais wa shirikisho la soka nchini humo Reinhard Grindel amethibitisha kocha huyo kuongeza mkataba huo ambao ulikuwa unafikia tamati 2020.

Hata hivyokupitia mtandao wa Twitter wa shirikisho hilo wameongeza kwa kuandika, “OFFICIAL: Joachim #Löw has extended his contract as [HASHTAG]#DieMannschaft[/HASHTAG] head coach until 2022! [emoji871] #Löw2022.”

Kocha Low alikuwa anatajwa kurithi kiti cha mzee Arsene Wenger kwenye klabu ya Arsenal.
 
Magufuli ampandisha cheo baada ya kushtukiza bandarini

MUUNGWANA BLOG / 33 minutes ago




Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kumpandisha cheo Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA bandari ya Dar es Salaam Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili bandarini hapo ndani ya wiki hii.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo wakati alipokuwa anazungumza viongozi mbalimbali kwenye bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwenye bandari na kusema amefanya hivyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Ben Usaje katika kusimamia maslahi ya nchi vizuri.

"Nawapongeza watu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi nzuri mnayoifanya, Waziri wa Fedha kampeni tu huyu ukamishna kamili kwa sababu amesimamia haki halisi kwaajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, najua wanamchukia sana wengine wafanyabiashara lakini waache wakuchukie Mungu anakupenda na watanzania tutaendelea kukupenda kwa hiyo mka-confirm. Katibu Mkuu mkazungumze wote mumpe angalau ndani ya wiki hii msimcheleweshe", amesema Dkt. Magufuli.

Uamuzi huo wa Rais Magufuli umekuja baada ya kumuuliza swali Kaimu Kamishna kuwa anafanya kazi gani TRA na ndipo alipotoa amri hiyo ya kupandishwa cheo haraka kutokana na kuwa ameweza kusimamia haki na maslahi kwa ufasaha.
 
Rais Magufuli aibua mapya bandarini

MUUNGWANA BLOG / 35 minutes ago




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Dkt. John Pombe Magufuli, leo amefanya ziara ya kushtukiza bandarini jijini Dar es salaam kukagua matanki ya mafuta ya kula, ambayo yameadimika hapa nchini.

Baada ya ziara hiyo na kufanya ukaguzi, Rais Magufuli amebaini kuwa kuna mafuta ambayo yameingizwa nchini huku kukiwa na taarifa za udanganyifu ili kukwepa kodi, yakiwemo mafuta ambayo yameshakamilika (refined oil) na kusema kuwa ni mafuta gahfi (crude oil).

Baada ya kugundua hilo Rais Magufuli amewataka wamiliki wa mafuta hayo kulipa ushuru wake unaostahili, pamoja na fine kutokana na udanganyifu walioufanya.

"Kwenye bidhaa walizosema ni crude kumbe ni refined oil walipe 25% pamoja na fine, hatuwezi tukawa tunaibiwa kila siku tunahitaji kujenga viwanda vetu, haiwezekani crude oil ukachaji sawa na semi refined, na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo, wabunge walipitisha kitu kingine, kinachojadiliwa kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupitishwa kuwa sheria kimebadilishwa kuwa kingine, "Hii crude oil ichajiwe bei ya juu ili watu wengi wajenge viwanda hapa ili tujenge nchi yetu ”, amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hilo Rais Magufuli amemtaka mkemia Mkuu wa Serikali kufuata maadili ya kazi, ili kuleta weledi na kujenga nchi.

"Mkemia Mkuu nataka sampo zozote mtakazokuwa mnapewa fanyeni kwa utaratibu kwa kuzingatia maadili, mkiletewa mkono wa albino semeni mkono wa albino msije mkasema mkono wa mbwa. Mkiletewa madawa ya kulevya semeni haya ni madawa ya kulevya sio unga wa muhogo, amesema Rais Magufuli.
 
Harusi ya mjukuu wa Malkia Prince Harry yapata pigo

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Kasri ya Kensington ambayo ni makazi rasmi ya mjukuu wa malkia wa Uingereza, Prince Harry na mchumba wake, Meghan Markle imetoa taarifa inayoashiria baba wa Markle ‘hatohudhuria sherehe ya harusi ya binti yake’.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Thomas Markle ambaye anatuhumiwa kupigwa picha za “paparazi” kwa makubaliano ya siri, amekataa kuhudhuria sherehe hiyo kwa kuhofia ‘kumuaibisha binti yake’.




Hata hivyo taarifa kutoka Kasri la Kensington zinadai Thomas Markle amepata shinikizo la damu.
 
Yeah!

Ila akija utasikia anaanza parabozi na misemo isiyo na kichwa wala miguu....

Bado kale kengine kabeba maua japo nako nahisi kameporomoshewa bonge la dedikesheni leo mchana...

Heshima kwa Jembekillo kwa sababu when all is said and done kuna watu humu watakuwa wanameremeta huku wakiwa wamepambwa maua...[emoji23][emoji23][emoji23]

[emoji445][emoji443][emoji444]Walisema haolewi mbona kaolewa[emoji444][emoji443][emoji445]
Yaani akianza yale manyimbo yake ndo huwa nachoka,sijui nan kamloga kwakweli.
Kayego kaoga kale[emoji23]
 
Kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite ametangaza majina 23 ya mwisho kwaajili ya fainali za Kombe la Dunia zinzotarajiwa kuanza June 14, 2018 nchini Urusi.

Brazil ambayo ipo E na timu za Costa Rica, Serbia na Switzerland, itacheza mechi yake ya kwanza Jumapili ya Juni 17. Nyota wa PSG Neymar ambaye ametoka majeruhi hivi karibuni ameitwa huku mlinzi Dan Alves akiachwa baada ya kuumia wiki iliyopita.

Mabingwa wa England Man City ndio timu ambayo imetoa wachezaji wengi kwenye kikosi hicho ikianza na mlinda mlango Ederson, mlinzi Danilo, kiungo Fernandinho na mshambuliaji Gabriel Jesus.

Kikosi Kamili:

Makipa: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).
Walinzi: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).

Viungo: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).
Washambuliaji: Neymar (PSG), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).
 
Msuva kung'ang'ana na TP Mazembe

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Ratiba ya mashindano ya klabu bingwa Afrika inaendelea leo ambapo mchezaji mtanzania Simon Msuva, ataingoza klabu yake Difaa El Jadidi ya nchini Morocco kupambana na timu ngumu ya TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi.

Mchezo huo wa pili wa kundi B utachezwa leo Mei 15, 2018, katika uwanja wa Stade Al Abdi huko Morocco kuanzia saa 4:00 usiku kwa muda wa Afrika mashariki.

Timu ya Difaa El Jadidi itahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka matumaini ya kusonga mbele baada ya mchezo wa kwanza kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya MC Alger kutoka nchini Algeria.

Mchezo mwingine wa kundi hilo utazikutanisha klabu ya ES Setif ambayo haina alama itawakaribisha wageni timu ya MC Alger

Katika msimamo wa kundi B timu ya TP Mazembe inaongoza ikiwa na alama 3 baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa magoli 4-1 dhidi ya timu ya Es Setif ya nchini Algeria

Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni pamoja na Swallows itakuwa mwenyeji wa timu ya De Agosto, KCCA FC dhidi ya Al Ahly, wakati timu ya ES Tunis wataikaribisha klabu ya Rollers na klabu ya WAC Casablanca itapambana na Togo Port.
 
Back
Top Bottom