Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NANI YUPO HATARINI KUPATA MARADHI HAYA?
Watu ambao wapo hatarini kupata magonjwa yasiyoambukiza ni wale ambapo wapo kwenye familia zenye historia ya magonjwa hayo, utaratibu wa maisha mtu anayoishi inaweza kuwa chanzo, hali ya mazingira mfano uchafuzi wa mazingira hasa kemikali za viwandani zinaweza kuwa chanzo. Uvutaji wa sigara pia ni chanzo kikubwa na takwimu zinaonesha kila mwaka takriban watu milioni tano hufariki kutokana na madhara ya tumbaku duniani kote.
 
Katika suala la mfumo wa maisha, watu wenye uzito mkubwa hufariki kutokana na maradhi yanayoambatana na uzito mkubwa na takriban watu milioni mbili na laki nane hufariki duniani kwa tatizo hili la ubonge.
Magonjwa haya yasiyoambukiza pia hutegemea umri wa mtu, jinsia na vinasaba na uchafuzi wa mazingira. Vilevile tabia inachangia sana mtu kupata maradhi haya. Mfano uvutaji wa sigara, kutokula chakula bora au kula vyakula vinavyonenepesha sana mwili na kutofanya mazoezi ya mwili halijalishi hata kama wewe ni mwembamba ni vema ufanye mazoezi. Kutofanya mazoezi na mlo usio wa afya kunaweza kukufanya uwe na kitambi na shinikizo la juu la damu. Hali hii itasababisha uandamwe na magonjwa mengi yasiyoambukiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…