Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

446424434_118430.jpg
 
Jukumu la kuwepo maisha bora katika jamii zetu linatuhusu wote bila kujali kiwango cha elimu ulichonacho, mali, umaarufu, udhaifu ulionao au imani uliyonayo. Tambua thamani yako na uitumie kutengeneza kumbukumbu yenye manufaa katika jamii yako. Unajua kila unachowafanyia watu huwa kinafyatua vipande vya kumbukumbu tofautitofauti kuhusu wewe!
 
Wakati mwingine tumekuwa tukiwalalamikia watu mbalimbali na wengine walikuwa watu wetu wa karibu kwamba wametuharibia maisha. Kwa mfano unaweza kusikia mtu akilalamika kuwa : “…… ameniharibia maisha yangu!”, “……..ameniaribia masomo yangu!” au “…….. amenifanya niitelekeze familia yangu!” na kadhalika. Lakini ni vizuri tukafahamu kuwa kila mmoja anawajibu wa kuilinda thamani yake aliyopewa na Mungu kabla ya wengine kuilinda na kuijali.
 
Umepokea ushauri wa watu wangapi wanaokushauri vibaya kuhusu malengo yako?
Uliwapa watu wangapi nafasi ya kuchezea muda wako!?
Umeenda maeneo mangapi yanayopunguza kasi ya kufikia ndoto zako!?
Umependa vingapi vinavyoondoa kusudi la thamani yako duniani!
 
Back
Top Bottom