Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Madhara

Kwa ujumla hali hii siyo ugonjwa na wala haihatarishi afya yako wala kuongeza uwezekano wa kuleta madhara zaidi kiafya. Ingawa hofu miongoni mwa waathirika wa hali hii ni jambo la kawaida kwa kuwa muonekano wa ulimi unaweza kuwa unakera kutegemea unavyoonekana kwa watu wengine.

Kingine kinachoweza kujitokeza ni ugumu wa kuhakikishiwa na daktari kwamba hali hiyo yenyewe siyo tatizo.
 
Tiba

Kwa kuwa hali hii siyo ugonjwa haihitaji matibabu yoyote isipokuwa inaposababisha kero na maumivu wakati wa kula baadhi ya vyakula, daktari anaweza kupendekeza dawa ili kuondoa usumbufu huo.

Daktari anaweza kupendekeza dawa za kuondoa maumivu, za kusukutua zenye ganzi fulani ndani yake au nyinginezo kutegemea na hali halisi iliyopo.
 
Unaweza, wewe mwenyewe, kupunguza adha ama kero ya hali hii kwa kujiepusha au kupunguza vitu vinavyoweza kuchochea kero zinazohusiana na hali hii kinywani kwa kuepuka vyakula ama vinywaji vya moto, vyenye pilipili, chumvi nyingi au vyenye asili ya tumbaku kama vile sigara.
 
BOSkd35D-XS.jpg
 
Mara nyingi vyakula tunavyokula huwa na faida mwilini lakini vingine huwa na madhara fulani ambayo sisi huwa hatuyajui hasa kama unashambuliwa na ugonjwa fulani.
Leo nimeona niliongelee hili kwenye safu hii maalum ya kukujuza jinsi ulavyo ndiyo matokeo ya baadaye.
Wapo wengi wanaosumbuliwa na suala la fangasi wa mdomoni lakini hawajui tiba wala sababu ya wao kupata ugonjwa huo.
 
Mara nyingi ugonjwa huu huwapata watoto wanaonyonya ingawa wao ni kawaida na mama huelezwa hospitali jinsi ya kufanya.
Ugonjwa huu ukitokea kwa wakubwa huwa si jambo la kawaida kwani husababisha mtu kujihisi vibaya kwa sababu wakati mwingine unaweza kujikuta ukinuka mdomo bila kujua tatizo na utando mweupe unaweza kukutoka, hii ni dalili kwamba umepata maambukizi.
Ni rahisi pia kuunguzwa na chakula hata kama hakikustahili kukuunguza kwa kiwango kikubwa, kwani ngozi ya ulimi inakuwa imeshashambuliwa na bakteria wa fangasi.
 
Vyakula vinavyosababisha fangasi:
Vyakula hivyo ni karanga, mayai, maziwa ya kawaida, maziwa mgando, yougurt ya baridi, vinywaji vyote nyenye kafeni kama vile kahawa, chai, chokoleti nk.
Vingine ni soseji nyama nyekundu, mayonnaise, salad, pia vyakula vyote vya baharini. Hivi ni vichache tunavyopendelea kula, kama wewe una tatizo la fangasi wa mdomoni nakusihi kuacha au kula kwa uchache vyakula hivyo wakati unatibu ugonjwa huu.
 
Vyakula tiba
Mdalasini ‘Cinnamon’:
Hiki ni kiungo kinatajwa kutibu moja kwa moja ugonywa huu, kwani kina uwezo wa kupigana na bakteria wanaoshambulia na wanaosababisha fangasi.
Jinsi mdalasini unavyoweza kutibu kama unapendelea kunywa yougurt, chukua unga wa mdalasini changanya kwenye yougurt yako kisha kunywa, pia unaweza kutumia chai ya mdalasini mara kwa mara.
Kama huwezi kuchanganya kwenye chai unaweza kuulamba unga wake kwenye asali asubuhi na jioni.
 
Jinsi yanavyotibu:
Pika chai kisha kiungo chako kiwe majani ya mzaituni, unaweza kuweka majani mawili mpaka matatu kwenye chai yako au ukipata majani ambayo yameshaandaliwa kama majani ya chai ni vizuri kwani yapo yanauzwa kwenye maduka makubwa ya vyakula. Kunywa chai kama tiba kwa siku mbili.
 
Mafuta ya nazi:
Mafuta ya nazi ni mazuri kama tiba. Hakikisha kwenye kila mlo wako unachanganya kijiko kimoja cha chai kama unao uwezo wa kupata mafuta hayo unaweza kuyafanya tiba ukatumia mafuta ya nazi ya ndani ‘Virgin coconut’ vijiko vitatu kwa siku.
 
Back
Top Bottom