Inapotokea sehemu ya papilla ikapotea katika sehemu kadhaa na kufanya maeneo husika kuwa na sura laini zaidi kwa kuitazama au hata kwa kuigusa na ambayo ni nyekundu zaidi ukilinganisha na sehemu nyingine za ulimi, na mipaka yake kuinuka kidogo huitwa, kitabibu, geographic tongue; ulimi kuwa na ramani. Ulimi kutengeneza maumbo yenye sura mfano wa ramani katika uso ni hali isiyo na madhara yoyote kiafya isipokuwa huweza kusababisha muonekano mbaya wa ulimi tofauti na unapokuwa haunayo.