MKE anadaiwa kumuua mumewe, Ahmed Salim kwa kumchoma kisu baada ya kumlazimisha kurudi jikoni kupika chakula baada ya kutoshiba mkoani Mtwara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, alisema tukio hilo lilitokea juzi mkoani humo ambapo mwanamume huyo alikufa papo hapo baada ya kuchomwa kisu na mke wake.
Alisema siku ya tukio majira ya saa 1:30 usiku, mwanamke huyo alimuandalia mume wake chakula na kumpatia.
“Kile chakula kilikuwa kidogo, mume wake, Ahmed Salim, alimtaka arudi jikoni kwa ajili ya kupika tena chakula kwa kuwa hakikumtosha. Hapo ndipo palitokea ugomvi wakalumbana na wakaendelea kugombana, mke alichukua kisu na kumchoma kifuani na kufariki dunia papo hapo baada ya kutokwa na damu nyingi kwenye jeraha.” alisema Kamanda Mkondya.