Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kweli tena, umpate anayejua maana ya upendo..Yaani maneno yake tu yanakufanya uipakate dunia.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kuipakata dunia tena....

Love is spirituality na inahappen mysterious way. Unaweza penda hata Jini for no reason ukiulizwa kwanini umependa kigagula wewe unabaki tu kujibu Nampenda hivo hivo tu.
 
Aidha, watafiti wanasema kuwa vipimo 1000 vya sumu kali aina ya (neo-nicotinoid) vinahitajika kuua kunguni katika maeneo mengine mbalimbali duniani, ambapo Watafiti hao wanasema kuwa kuna hatari kubwa ya mdudu huyo kuenea kote duniani kutokana na utandawazi na soko huria ambao umefanya ulimwengu kuwa kitongoji kikubwa tu.
 
CHIMBUKO:
KUFIKIA katikati ya karne ya 20, ilionekana kwamba wanadamu wamefaulu kuwadhibiti kunguni, lakini uhalisia ilikuwa ni kuwapunguza tu na sio kwateketeza kabisa.
Watu fulani zamani waliwafahamu kunguni kupitia tu wimbo wa zamani wa Kiingereza ulioimbwa na watoto wa shule za nasari (au chekechea) uliosema: “Usiwaache kunguni wakuume.”
 
Hata hivyo, katika miaka ya 1970, nchi nyingi ziliamua kupiga marufuku matumizi ya dawa ya DDT— ambayo iliyokuwa dawa kuu ya kuulia kunguni kwa kuwa ilikuwa pekee yenye sumu kali na iliyoharibu mazingira kwa ujumla wake ikiwemo kuweza kuleta madhara kwa wanadamu pia.
 
Lakini kiuhalisia kunguni, ametokea katika chimbuko la wadudu watambaao wenye pingili na huelezwa chanzo chao kikuu ni uchafu uliogandamana na kutengeneza baikteria ambao nao hubadili tabia siku kadiri ya siku, kama ilivyo kwa kinyesi cha kuku ukikifunika na kikianza kuvunda kwa joto utapata wadudu wa mfano huu wa kunguni wenye pingili (weupe)
 
Hata hivyo, kemikali nyingine zilipotumiwa ilionekana kwamba kunguni walikuwa sugu na hazikuweza kuwaua, ila zilisaidia kuwapunguzia tu kasi ya kutoka kwa wingi kwenda kushambulia wenyeji wao usiku.
Pia watu walianza kusafiri mara nyingi zaidi na bila kujua walihama pamoja nao. Matokeo yakawaje? Ripoti moja ya mwaka wa 2012 kuhusu kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita kunguni wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati, nchi kadhaa za Ulaya, Australia, Afrika mashariki zaidi kuripotiwa ilikuwa maeneo (kaunti) za Kisumu, Nakuru Kenya na maeneo kadhaa Tanzania na uganda.”
 
Awali jijini Moscow, Urusi, katika mwaka mmoja hivi karibuni, ripoti za kutokea kwa kunguni ziliongezeka mara kumi kuliko ilivyokuwa hapo awali, na Wakati huohuo, upande ule mwingine wa ulimwengu, huko Australia, kumekuwa na ongezeko la asilimia 5,000 la kunguni tangu mwaka wa 1999!
Watu fulani hubeba kunguni bila kujua wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa hoteli nchini Marekani, “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni wataendelea kuwapo.”
 
SWALI KUBWA KWA WATU KWA HIVI SASA NI KUWA NI:
Kwa nini ni vigumu kiasi hicho kuwamaliza kunguni?
Unaweza kujilindaje dhidi yao?
Na je Kunguni wanapoivamia nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia wasirudi tena?
Aidha wanasayansi wa Jarida la ENTOMOLOGY wanashauri kutafutwa mbinu tofauti na iliyo mpya ya kaajili ya kukabiliana na kunguni hao pasipo kutumia sumu zenye madhara kwa mazingira, badala yake kuzalishwe wadudu wengine wanaoweza kuwala kunguni ili kuwazuia wadudu hawa kuendea kuenea kwa kwasi ya hivi sasa maeneo mbalimbali duniani.
 
HII MUHIMU ZAIDI KUFAHAMU,
JE WAJUA: Kunguni hawa huweza kustahimili kukaa muda mrefu pasipo kufyonza damu ambayo ni chakula chao kikuu, Yaani wadudu hawa wakivamia nyumba yako na ukasema unahama kwa muda ili ukirudi wawe wametokomea, ukweli ni kuwa “Unajidanganya” hata ukae miezi sita ukirudi utawakuta tena sasa wakiwa kijiji... hahahah!
 
Kwanza kunguni Ni Wadudu Wasiokufa kwa Urahisi
Hii ni kwa kuwa wadudu hao ni wadogo kama mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha mahali popote pale, ikiwemo katika godoro lako, fanicha zako, sehemu ya ukutani ya kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako.
Kwa kawaida kunguni hupenda kujificha mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na maeneo ya kuketi.
 
Mara nyingi, kunguni huwauma watu wanapolala, Hata hivyo watu wengi hawahisi maumivu wakishadungwa (wanapoumwa) kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha kinachomwezesha kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa.
Na ingawa wengi hudhani kunguni wanaweza kula kila siku, lakini ni tofauti zaidi kwani tafiti mbalimbali zanaonyesha kuwa, kunguni akishakunywa damu ya kutosha huweza kuitumia hiyohiyo kwa takribani siku4-7, na hii inamaanisha kwamba wingi wa kunguni huchochea kila siku kuhisi unang’atwa na wadudu hawa.
 
Na kipindi hicho cha wiki kinapopita pasipo kupata damu, haiwadhuru sana kwani wanaweza kuendelea kuishi bila kula kwa miezi mingi hata karibia na mwaka kwa kuendelea kula virutubisho vingine vipatikanavyo kwa wadudu wengine au hata katika mavumbi na utando mwingine wa uchafu vyumbani uwavutao wadudu wengine watambaao.
Hivyo njia kuu ya kupambana nao ni kuweka mazingira safi ya nyumba na, kuhama kwa muda, na wasipopata damu basi hufunga safari kuondoka eneo hilo.
PILI:
Kunguni jike mmoja huweza kuzalisha mamia wengine kwa juma moja tu
 
Tafiti kuhusu wadudu hawa zinaonyesha kumbeba kunguni mmoja tu, na kumleta nyumbani mwako, huweza kuwazalisha wengine zaidi ya mamia endapo watakutana na mazingira rafiki kwao ya uchafu, kwani inasemekana jike mmoja wa kunguni huweza kutaga mayai zaidi ya 10 kwasiku sawa na 80 kwa wiki na kuyaangua yote, hivyo na mtoto jike aliyeanguliwa humchukua siku18-21 na yeye kutaga mayai mengine.
Hebu fikiria wameanguliwa 80 kwa wiki, na baada ya wiki tatu kati ya hao 80, jike ni 40, nao 40 wakaangua 80 kila mmoja..?! wanapatikana wangapi?
Tofauti na mbu na wadudu wengine, inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya kuambukiza, Hata hivyo, wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu hiyo inavimba, na watu wengi huweza kuathiriwa kihisia au kuweweseka mara kwa mara usiki, kukosa kujiamini mbele ya wenzao nk.
 
VUTA PICHA: “unaathirika kisaikolojia kwanini..?” kwa kuwa kunguni wanatabia ya kunata kwenye pindo za nguo, na pindi unapoivaa nao huwepo, hivyo pindi unapotembea nao na kwenda mazingira tofauti, nao huambua na kuanza kuhama au kutoka sehemu waliyokuwepo na kuzurura ili kutafuta sehemu nyingine iliyosalama zaidi kwao kujificha.
Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka, Jarida moja nchini Sierra Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…