Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nimewahi kufanya jaribio la kuwauliza watu wengi kama wanaishi kwa furaha, lakini wengi wao walinijibu kuwa hawana furaha maishani mwao.

Hapo nikamkumbuka rafiki yangu “Masumbuko”, Hili siyo jina lake bali amepachikwa na watu kutokana na tabia yake ya kulitumia neno hili kila mara.

Kinachonishangaza ni kuwa kila ninapokutana naye huonekana hana furaha na ninapomuuliza kipi kimsikitishacho huwa hakosi sababu.
 
Mara nyingi huzungumzia matatizo ya kazini, siku nyingine ya nyumbani kwake na mara nyingine hutaja changamoto zinazotokana na mambo ya kijijini kwake.

Kila anaposalimiwa na kuulizwa hali yake hujibu kwa kusema; maisha yangu ni masuumbuko tu wala sina furaha.

Siku moja nikamuuliza “Unafikiri masumbuko yako yataisha lini?” Alinijibu,“Bwana nimekata tamaa”.
 
Kuna wakati niliwaza kuwa yatakwisha nitakapojenga nyumba yangu, au wakati watoto wangu watakapomaliza shule na kuanza kazi au wakati nitakapostaafu na kujiajiri mwenyewe kwa kuendesha miradi.

Lakini kila nilililoliwazia linapotimia bado maisha yangu yanaendelea kuwa ya masumbuko.

Huenda kuna watu wengine wenye mawazo kama ya rafiki yangu Masumbuko.
 
Upendo + mapenzi + wapendanao + furaha + Amani = RAHA TUPU.[emoji177][emoji177][emoji177][emoji177]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…