Robo fainali sasa itapigwa leo Ijumaa na kesho Jumamosi, ambapo timu zitakazohusika ni Uruguay, Ufaransa, Brazil, Ubelgiji, Russia, Croatia, Sweden na England, ambazo zitapambana kuwania kuingia kwenye nne bora. Wakati fainali hizo zikiwa zimefikia kwenye nane bora, Ligi Kuu England ina wachezaji kibao waliobaki, licha ya kuondoshwa kwa majina makubwa kama kama Mohamed Salah, Sergio Aguero na David de Gea. Mastaa wengine wakubwa waliotupwa nje ni Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Lakini, hizi hapa ndiyo klabu zenye wachezaji wengi waliofika hatua ya robo fainali na timu zao kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia 2018 huko Russia.