Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

OLIVIER Giroud ametimiza ahadi yake ya kunyoa aliyokuwa ameitoa kama Ufaransa itashinda ubingwa wa Kombe la Dunia 2018 huko Russia. Kabla ya fainali hizo kuanza, wachezaji kadhaa wa Ufaransa walitoa ahadi ya kufanya mambo fulani kama timu yao itabeba ubingwa.

Giroud, Nabil Fekir na Hugo Lloris walitoa ahadi ya kunyoa, wakati Blaise Matuidi aliahidi ataendeesha baiskeli kutoka Paris, Ufaransa hadi Turin, Italia.
 
HALI tete pale Ujerumani. Matokeo yao mabaya Kombe la Dunia pale Russia hayajawahi kuwaacha salama. Bundi anaunguruma na sasa kiungo, Mesut Ozil ameachana na Timu ya Taifa ya Ujerumani huku akiwachana vibaya mabosi wa soka la Ujerumani.

Ozil ametoa shutuma kali kwa mabosi wa Shirikisho la soka la Ujerumani, DFB huku akiwashutumu kwa kumbagua na kumfanya kisingizio cha matokeo mabovu ya Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia.
 
Staa huyo wa Arsenal ambaye alipaa na kikosi cha Arsenal juzi kwenda Singapore kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya amedai hajisikii kuvaa tena jezi ya Ujerumani licha ya kuwa na umri wa miaka 29 tu.
 
Nahisi sitakiwi na nadhani mafanikio niliyopata na Ujerumani tangu nilipoichezea mechi ya kwanza mwaka 2009 yamesahauliwa. Sitaichezea tena Ujerumani katika soka la kimataifa huku nikiwa na hisia nabaguliwa na siheshimiwi. Nilizoea kuvaa jezi ya Ujerumani huku nikisikia fahari na raha, lakini sio sasa hivi,” alisema Ozil.
 
Wakati mabosi wa ngazi za juu wa DFB wakinifanyia walichonifanyia, kutoheshimu asili yangu ya Uturuki, kibinafsi zaidi kunigeuza kama ajenda ya kisiasa, basi tufanye imetosha. Hii sio namna ambayo mimi nacheza soka na sitakaa kimya na kutofanya lolote. Ubaguzi wa rangi kamwe haukubaliki,” aliongeza Ozil.
 
Tukishinda nakuwa Mjerumani, lakini tukifungwa nakuwa mhamiaji. Sitakubali kuendelea kuwa kisingizio kwa sababu ya uzembe wao wa uwajibikaji. Kuna sifa yoyote ya kuwa Mjerumani kamili ambayo sina? Rafiki zangu Lukas Podolski na Miroslav Klose kamwe hawajawahi kuchukuliwa kama Wajerumani Wapoland, mbona mimi nachukuliwa kama Mjerumani Mturuki? Ni kwa sababu nina asili ya Uturuki? Ni kwa sababu mimi ni Muislamu?” alihoji Ozil.
 
Mapema kabla ya kutangaza kustaafu kuichezea Ujerumani, Ozil alijitetea kutokana na kitendo chake cha kupiga picha na Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan na kumpatia jezi ya Arsenal jijini London mwishoni mwa msimu uliopita huku akidai kama angekataa fursa hiyo angekuwa amedharau asili yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…