Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Muingereza Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018.
Eden Hazard wa Chelsea, Mohamed Salah kutoka Liverpool,Kevin De Bruyne wa Manchester City na mshambuliaji mpya wa Juventus Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa waliojumuishwa.
Lucy Bronze kutoka Uingereza pia amejumuishwa katika tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.
 
Alishiriki michuano hii ya kombe la dunia akiwa tiyari na magoli 30 kwenye ligi kuu England.
Aliweza pia kuwa na kiwango kizuri katika michuano ya kombe la dunia, akiwa mchezaji wa kwanza kutoka England kushinda kiatu cha dhahabu tokea alivyofanya Gary Lineker mwaka 1986.
 
Hazard mwenye miaka 27 alishinda kikombe cha FA akiwa na Chelsea mwezi May na pia kuifikisha timu ya Ubelgiji katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya kombe la dunia ikiwa ndio nafasi nzuri zaidi kwa Ubelgiji kuifikia tokea kuanza kwa mashindano haya.
Salah mwenye miaka 26 alikua pia na msimu mzuri ndani ya Liverpool. Raia huyu wa Misri alifunga magoli 46 kwa upande wa klabu na kwenye timu ya taifa, huku pia akiifikisha Liverpool katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.
 
Walioorodheshwa
Cristiano Ronaldo - Juventus & Ureno
Kevin De Bruyne - Manchester City & Ubelgiji
Antoine Griezmann - Atletico Madrid & Ufaransa
Eden Hazard - Chelsea & Ubelgiji
Harry Kane - Tottenham & England
Kylian Mbappe - Paris St-Germain & Ufaransa
Lionel Messi - Barcelona & Argentina
Luka Modric - Real Madrid & Croatia
Mohamed Salah - Liverpool & Misri
Raphael Varane - Real Madrid & Ufaransa
 
Kwa upande wake De Bruyne mwenye miaka 27 alikua na mchango mkubwa sana katika rekodi nzuri iliyowekwa na klabu yake ya Manchester City kwa kufikisha alama 100 na kuipa ubingwa wa EPL. Alifanya vyema pia akiwa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji iliyoibuka mshindi wa tatu kwenye kombe la dunia 2018.
Ulikuwa mwaka mzuri pia kwa mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo. Mreno huyu alifunga magoli 54 katika michezo 54 ya michuano yote, akiipa pia klabu yake za zamani Real Madrid kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo.
Mwisho wa kupiga kura utakua Agosti 10 na tuzo zitatolewa mjini London Septemba 20.
 
Back
Top Bottom