Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ozil na staa mwingine wa Ujerumani, Ilkay Gundogan walikuwa wameshutumiwa Ujerumani kwa kukutana na rais huyo pamoja na mshambuliaji wa Everton, Cenk Tosun wakati huu rais huyo akishutumiwa kwa udikteta huku pia ziara yake jijini London ikimkutanisha na waandamanaji wa haki za binadamu.
 
Kustaafu kwa Ozil katika timu ya taifa kumezua gumzo kubwa kwa mashabiki wa soka la Ujerumani lakini hakujapita hivi hivi. Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness amedai ni afadhali Ozil amestaafu timu ya taifa kwa sababu alikuwa mzigo.
 
Nina furaha jambo hili limekwisha. Amekuwa akicheza ovyo kwa miaka mingi. Mara ya mwisho aliupora mpira kwa adui kabla ya Kombe la Dunia 2014. Kwa sasa anajaribu kuficha kiwango chake cha ovyo kwa kutumia hiyo picha na Rais,” alisema Hoeness. “Popote sisi Bayern tulipocheza na Arsenal tulimlenga yeye kwa sababu tulijua ndio udhaifu wao ulipo.
 
Ana wafuasi milioni 35 mitandaoni na wanaamini anacheza vizuri pale tu anapopiga pasi iliyofika. Maendeleo katika soka letu ni majanga. Inabidi urudi nyuma na kuujua mchezo huu ulipo. Na kwa mtazamo wa kisoka, Ozil hakupaswa kuwa na nafasi timu ya taifa kwa miaka mingi sasa.”
 
Ozil aliichezea Ujerumani mechi ya kwanza chini ya kocha wa sasa, Joachim Low Februari 2009. Kuanzia hapo alicheza mechi 92 na kufunga mabao 23 mpaka juzi alipotangaza kustaafu. Kumbukumbu kubwa katika maisha yake ya soka ngazi ya kimataifa inabakia kuwa taji la Kombe la Dunia walilotwaa na wenzake kule Brazil mwaka 2014.
 
Martial anafahamu wazi jina lake linatajwa huko Chelsea, linatajwa huko Tottenham Hotspur, hivyo anaamini akisema aachane tu na Manchester United atapata ofa ya kwenda kujiunga na timu kubwa ambazo zina uwezo wa kushindania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao. Kuna wakati fowadi huyo wa zamani wa AS Monaco alihusishwa na Juventus, lakini Mourinho ametoa kauli iliyoibua utata mkubwa. Kwamba hataki Martial aondoke, au ataenda ambako siko anakotaka kwenda? Hilo ni swali.
 
Taarifa za ndani kwenye klabu hiyo ya Man United zinafichua Mourinho yupo tayari kumuachia Martial aondoke kwenye kikosi chake, lakini kwa masharti mawili makubwa. Kwanza kwenye meza kuwepo na ofa inayozidi Pauni 60 milioni, ambayo itawafanya kupata faida kwenye mauzo na zitakuwa pesa zitakayowapa uwezo wa kwenda kumsajili mbadala wake, Ivan Perisic.
 
Sharti la pili ni kwamba amemwambia bosi Ed Woodward Martial akiuzwa, auzwe tu, lakini si kwa timu ya Ligi Kuu England.

Hiyo ina maana kama Juventus au klabu nyingine yoyote ya nje ya England, ikileta Pauni 60 milioni, itambeba staa huyo wa Ufaransa. Chelsea inapiga hesabu za kuinasa huduma ya Martial ikiwa ni maandalizi yake ya kumbadili Eden Hazard kama atakwenda Real Madrid.
 
Mourinho ametema cheche kuhusu kiungo wake Paul Pogba. Supastaa huyo wa kimataifa wa Ufaransa siku za karibuni amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Barcelona, lakini kocha huyo Mreno alisema hatasimama kwenye kizingiti na kumzuia mchezaji huyo asiende Nou Camp kama tu kwenye dili lake litamhusisha kiungo Ivan Rakitic. Mourinho alisema Barcelona ikiliweka jina la Rakitic kwenye mpango huo wa kubadilishana na Pogba pamoja na pesa juu, hatapinga atafanya biashara safi kabisa.
 
[emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji870][emoji870][emoji870][emoji870][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji870][emoji870]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…