Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watumiaji wengi wa simu hawapendi usumbufu usiokuwa na manufaa kwao kwa kuwa kwa bahati mbaya matangazo hayo yanatumwa pasipo kuzingatia mahitaji na matakwa ya mteja

Katika mitandao ya kijamii watumiaji wamekuwa wakijibizana na watoa huduma (kampuni za simu) hususan watumiaji wanapoibua hoja ya kukerwa na matangazo hayo, lakini majibu ya kampuni yamekuwa ya kujing’atang’ata.
 
Hatua hiyo inaonyesha asilimia kubwa ya watumiaji wa simu na pengine wote hawafurahii matangazo hayo ambayo wakati mwingine yanamlazimu mmiliki kuacha shughuli zake za msingi ili kuitika mwito wa simu, lakini anakutana na matangazo ya michezo ya kubahatisha ambao hajawahi hata kufikiria kuwa ipo siku atashiriki.

Nadhani kuna biashara inaendelea kati ya mitandao ya simu na wale wanaopigiwa debe na bila shaka inaingiza kiasi kikubwa cha fedha, ndiyo maana wanakumbatia jambo hili ambalo kwa watumiaji wa simu halina maana wala manufaa yoyote.
 
Kimsingi fedha hizo zinazovunwa kupitia matangazo hayo zinapaswa kugawiwa kwa wateja kwani wao ndiyo wamegeuzwa ubao wa matangazo kwa kuwa yakitangazwa mahali pengine ni lazima yatatakiwa kulipiwa.

Jicho la pili katika kero hii ni kwamba inasababisha kupotea kwa mapato ya kampuni za matangazo na vyombo vya habari na kuikosesha Serikali mapato ya kodi yanayotokana na matangazo hayo.
 
TCRA mnapaswa kuchukua hatua juu ya tabia hii ambayo kwa sasa inaota mizizi ili kuondoa kero hii kwa wananchi na kunusuru mapato yanayopotea.

Watumiaji wa mitandao nchini licha ya kushindwa kuchukua hatua ya kujinusuru na kero hiyo, hawafurahishwi na matangazo na nyie kwa nafasi yenu mnaweza kuwakataza mnaowasimamia.

Watoa huduma nao mnapaswa kufahamu kuwa matangazo mnayowapatia wateja wenu si lengo lao la kununua simu na wanajua ni wapi watapata matangazo hayo.
 
Kuchukua matangazo ya kibiashara na kuyaleta kwenye simu za watu moja kwa moja ni kinyume cha mahitaji ya watumiaji wa simu.

Waacheni wenye matangazo wayapeleke kunakohusika kwa ajili ya kutangazwa lakini si nyie kujitwika majukumu hayo kwa kuwa mnajua mtayatupa kwenye simu za watu.
 
Na kama mnalipwa, basi kuwepo mgawo mtakaoutoa kwa watumiaji wa mitandao yenu kwa sababu ya kuwalazimisha kusikiliza au kusoma ujumbe mnaowatumia kupitia simu zao ilhali hawakuukusudia.
 
Na kama mnalipwa, basi kuwepo mgawo mtakaoutoa kwa watumiaji wa mitandao yenu kwa sababu ya kuwalazimisha kusikiliza au kusoma ujumbe mnaowatumia kupitia simu zao ilhali hawakuukusudia.
 
Siku moja baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kueleza kuwa imeanza kuziondoa dawa za kutibu shinikizo la juu la damu (presha) aina ya Dyanaval zilizobainika kusababisha saratani, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imesema haihusiki na uingizaji au usambazaji wa dawa hizo.

Juzi, TFDA ilisema imeanza kuziondoa sokoni dawa hizo na shughuli hiyo ilianza Ijumaa ya wiki iliyopita na itafanyika ndani ya siku 14.

Akizungumza na Mwananchi jana, Msemaji wa MSD, Etty Kusiluka alisema dawa ya kutibu presha ambayo wamekuwa wakiiagiza ni Valsartan ambayo huagizwa nchini India na Swizerland.
 
Hiyo ni tofauti kabisa na iliyopigwa marufuku na TFDA ambayo sisi hatujawahi kuiingiza na hata zilizopo kwenye mzunguko vituo vya afya na hospitalini ni Valsartan ambayo ina kiambata hai,” alisema Kusiluka.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa dawa hiyo nchini, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema inapotokea dawa kuwa na ubora hafifu mamlaka ya dawa na chakula huchukua hatua za kuiondoa katika mzunguko.

“TFDA imekuwa ikiendelea kufanyia tathmini dawa zote zinazoingia nchini, ikiwa dawa itaonekana haina ubora wa kutosha itaondolewa sokoni ili kuendelea kulinda afya za Watanzania,” alisema Waziri Mwalimu.
 
Dawa hizo, Dynaval Co 80 / 12,5mg, Dynaval Co 160/ 12.5mg na Dynaval Co 160 /25mg; pia hutambulika kwa jina la soko la Valsartan Co, au Hydrochlrothiazide.

Dawa hizo zinazozalishwa China, zimeshapigwa marufuku na kuondolewa sokoni katika nchi za Afrika Kusini, Marekani, na Uingereza.

Taarifa ya TFDA iliyotolewa jana inaeleza kuwa imewataka wagonjwa wa shinikizo la damu kuacha kuzitumia dawa hizo na kwenda kwenye vituo vya afya ili wabadilishwe dawa.
 
Wamiliki wa maduka ya dawa wametakiwa kurudisha dawa hizo kwa wasambazaji wa dawa hizo,” inaeleza taarifa.

Pia taarifa hiyo iliwataka watalaamu wa afya kuacha kuwaandikia dawa aina hiyo wagonjwa na badala yake watumie ile iliyosajiliwa na TFDA.

“TFDA imesajili dawa nyingine ya kutibu shinikizo la damu yenye viambato vya Varsaltan ambayo ni salama,” inaeleza taarifa hiyo.
 
Back
Top Bottom