Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

DDBE3D1E-78A4-43B4-984E-1F1FF4031BEC.jpeg
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ,,umesahau eeh?? Mlimaji mmoja, mvunaji mmoja ila kwenye kula sio mmoja tena,,, tunakula wengi
Mbona hatukaribishani sasa? Tukaribishane bwana tujumuike pamoja kula matunda ya nguvu zako ulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu..Wengine tulipewa nguvu za kutafuna tu[emoji23]
 
Julai umekwisha na Agosti imeanza kushika na kasi ya usajili imepamba moto, ususani katika sehemu ambazo usajili utafungwa mapema kama Ligi Kuu England.
Klabu kubwa Ulaya zinajitaidi kuhakisha zinakamilisha usajili wao mapema kabla ya jua kuzama.
Hapa tunaangalia jinsi klabu mbalimbali zinavyojaribu kuhimalisha vikosi vyao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
 
Real Madrid
Tayari Real ‘Los Blancos’ wamewasajili Vinicius Junior, Andriy Lunin na Alvaro Odriozola, lakini kuondoka kwa Cristiano Ronaldo inawalazimisha kutafuta mshambuliaji mwingine wa kati.

Harry Kane, Mauro Icardi na Robert Lewandowski wamekuwa wakihusishwa na kutaka kujiunga na Real, lakini kilichobaki ni kuona kama kweli wachezaji hao watatu watafanikisha uhamisho huo.
Real Madrid pia inatafuta kipa mwingine na Thibaut Courtoishas amekuwa akihusishwa na kuhama pamoja na nyota mwenzake wa Chelsea, Eden Hazard wamehusishwa kujiunga na miamba hiyo.
 
Barcelona
Ernesto Valverde alisema wakati wa ziara ya Barcelona kuwa anataka kiungo mwingine wa kuziba pengo la kuondoka kwa Andres Iniesta na Paulinho.
Tayari Arthur na Malcom wamesajiliwa, pia ameongeza beki mwingine wa kati Clement Lenglet, lakini bado Barca wanaonekana wanamtaka kiungo mmoja kati ya Willian, Adrien Rabiot na Paul Pogba wote wamekuwa wakihusishwa na kutakiwa Camp Nou.
 
Atletico Madrid
Diego Simeone tayari ameshaitegeneza Atletico Madrid kwa kuwanunua Thomas Lemar, Gelson Martins, Rodri na Santiago Arias, lakini anataka kuongezea nguvu kidogo.
Taarifa zinasema Luciano Vietto na Kevin Gameiro wote wanapewa nafasi ya kujiunga na miamba hiyo.
 
Manchester City
Mabingwa wa England wanaonekana wamemaliza usajili wao mapema, wakiwa wamezipata saini za Riyad Mahrez na Philippe Sandler.
Wamemaliza biashara yao, labda itoke nafasi ya kipekee au waondokewe na mchezaji na kulazimika kuziba pengo hilo.
 
Back
Top Bottom