CHANZO CHA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU NI KUMPENDA MUNGU.
Kumpenda Mungu ni kuitii sauti yake Bwana Mungu kwa bidii,kufanya maagizo yake yote na kutembea katika sheria zake zote.
*Mungu anachokiitaji kwetu sisi wanadamu ni kitu kimoja tu,nacho ni kurejesha Ushirika wa Roho mtakatifu ndani yetu ili kuruhusu NENO lake lipate nafasi ndani yetu.Maana kusudi kuu la kuumbwa kwa mwanadamu ni kukaa katika UWEPO wake/Ushirika wa Roho Mtakatifu.
Na ndio maana Bwana Mungu akaacha ENZI na MAMLAKA,akashuka mpaka chini ili amkomboe mtu aliyepoteza USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU.
Hivyo Bwana Mungu anachokihitaji kwako ni KUMPENDA YEYE.
Kumbu.10:12
“ Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na KUMPENDA , na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;”
*Mpenyo wa mwamini upo katika kumpenda Mungu, Ushirika wa mkristo upo katika Kumpenda Mungu.
*Mtu anayetaka USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU kwanza lazima akamatwe na PENZI maana penzi hulipwa kwa penzi.
-Tazama hata tu kwa mpenzi wako wakawaida ,ile namna unavyojisikia kuongea naye mara kwa mara,yaani ile kama hujamuona tu,
ni lazima utajisikia vibaya,Na ndio hali ilivyo kwa Yule anayempenda Mungu,
Kamwe hawezi kukaa mbali na UWEPO wa Mungu,Kamwe hawezi kukaa pasipo kuwasiliana na Mungu kwa njia ya Maombi.
*Amua kumpenda Mungu kwa kuomba NEEMA YA PENZI KWA MUNGU ili UKAE KATIKA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU mahali ambapo kuna Ushindi ,
Maisha ya kweli,
Kuinuliwa,
Kufanikiwa kiroho hata kimwili maana sisi tumeumbwa ili tuwe watu safi kila eneo la kiroho hata kimwili.
MBARIKIWE.