Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1525593987810.jpg
 
Yaani sasa hivi ukipata malaria hakuna dawa zaidi ya mseto,mjiandae[emoji124][emoji124][emoji124]
Mara ya mwisho kuumwa malaria ni mwaka 2001,wakasema nina sijui nini 14+. Tangu nina akili zangu ndio ilikuwa mara ya kwanza kulambwa sindano za dripu, baada ya siku tatu nesi akaja na trei lake... "Kyusa geuza tako ulambishwe[emoji382] [emoji382]" weeee!!!! Hapakutosha. Kikao kika kaliwa, hatimaye vikatafutwa vidonge nimesahau jina ni vya Kichina
 
Shem wewe ni muoga wa sindano khaa!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nakumbuka mama alinipeleka hospitali (bahati ni kwamba nyumbani na hospitali ya wilaya tulitenganishwa na seng'enge) tukapima vizuri ile ya kuchanja kidole halafu damu unapaka kwenye ki glass. Kumbe nina malaria, tukahamia benchi lingine. Ile tunasogea tunafuata mlango wa chumba cha sindano, baba mkubwa (rip) alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kunikaba ili nichomwe sindano,mimi nikashituka.

Baba mkubwa akaniletea peremende, sio kawaida yake, nikasema tu "mfwile lilino bhibhi gwanghu ulikughu bhikungogha... "

Ghafla nikanyamaza nikaomba niende chooni (huko kwenye chumba cha sindano ni kilio kimetawala cha watoto na majiko ya stovu ya kuchemshia sindano yanasikika kwa nguvu) nikakojoe, mama (rip) akagoma,nikavua kaptula na chupi nikamuomba anishikie kama haniamini. Yaani hapo ni mimi,shati na fenesi langu nimelishikiria na mkono wa kushoto nalia. Watu wakasema mwache akakojoe...
Ile kuniruhusu tu....
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] mama alinikuta nyumbani nimejifungia ndani.

Na uzee wangu huu, sipo tayari kuchomwa sindano ya aina yoyote ile
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom