Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Kibeta, Respicius Patrick (50) kwa tuhuma za mauaji, baada ya kumchapa mwanafunzi wa darasa la tano wa shule hiyo, Siperius Eradius na kusababisha kifo chake.
Akizungumza leo Jumanne Agosti 28, 2018 kamanda wa polisi mkoani Kagera, Augustino Ollomi amesema kifo cha mwanafunzi huyo kimetokea jana wakati akipelekwa hospitali.
Amesema marehemu alipelekwa kwa Patrick ambaye ni mwalimu wa nidhamu na mwalimu mwingine wa shule hiyo, Herieth Gerard (46), aliyedai kupotelewa na mkoba wake.