Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. MAHITAJI YALOTUMIWA: Kawaida, mahitaji yanayotumika kwa upishi wa keki ni : Unga, mayai,siagi, na sukari. Lakini sio keki zote zinapikwa kutumia mahitaji haya. Yanaweza kupungua au kuzidiwa. Mifano ya keki ambazo zinatofautiana kwa mahitaji ya :
 
2.MATAYARISHO YAKE: Keki pia zinatofautiana kwenye matayarisho yake. Hii inasababishwa na mahitaji ambayo mtu atatumia na keki inayopikwa. Kwa mfano keki ambazo haziwekwi baking powder (kwa mfano SPONGE CAKE), matayarisho yake ni tofauti na keki ambazo zinawekwa baking powder (kwa mfano BUTTER CAKE).
 
4.LADHA NA HARUFU ZINAZOTUMIWA: Keki huongezwa ladha na harufu tofauti kwa mfano cocoa kutengeza keki za chokoleti, au unga wa kahawa kidogo kuleta harufu ya kahawa kwenye keki, arki/essense au matunda (kwa mfano ndizi kwenye banana cake, zabibu, maganda ya ndimu au machungwa, nk)
 
6.KILICHOTUMIWA KUPAMBIA KEKI: Upambaji wa keki nao unaweza kutumia aina tofauti ya bidhaa za upambaji keki aidha ndani ya keki yenyewe au kwa juu kwa mfano BUTTER CREAM (krimu), ROYAL ICING, FONDANT (kwa mfano keki za harusi), JAMS/PRESERVES (kwa mfano swiss rolls), CHOCOLATES, nk
 
7. UMBO LA KEKI: Kila keki nayo inakuwa na umbo lake tofauti. Zipo keki ambazo zimepangwa na kushikanishwa kama vile mikate iloshikanishwa kwa siagi ili iwe keki moja lakini ndefu kwa urefu wake (SANDWICH CAKES/LAYER CAKES) na zipo keki ambazo ni moja tu nene haina mgao aina yoyote katikati, Pia shepu ya keki inaweza kutofautiana kwa mfano zipo zenye umbo la duara, mraba, nene,fupi nk.
Pia kuna keki ambazo zinakuwa na daraja mbili tatu (au zaidi) kulingana na sherehe iliyopikiwa hizi nazo zinaitwa (TIER CAKES).kwa mfano keki za harusi.
 
ANGAZO: Kwa hivyo kumbuka, keki hiyo hiyo moja inaweza kuwa kwenye kundi moja, mbili au yote kulingana na mahitaji yake, matayarisho yake, ladha yake, upambaji wake au umbo lake! Unapoenda kununua keki ya shughuli au harusi, zijue tofauti zake ili ufahamu na ujue unanunua nini na kwa nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…