moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 159,165
- 777,891
Huyu ni Isabel Dos Santos. Ni binti wa aliyekuwa rais wa muda mrefu wa Angola Eduardo Dos Santos. Enzi za baba yake alitajirika sana kwa sababu makampuni yake ndiyo yalikuwa yanapatiwa tenda kubwa kubwa zote mpaka akafanikiwa kuwa Oprah Winfrey wa Afrika - mwanamke tajiri kuliko wote Afrika. Kwa sasa anatumiwa kama mfano mbovu kuelezea dhana kwamba ufisadi (ukiwemo ule wa kutisha) hauchagui jinsia na hata wanawake wakiwezeshwa wanaweza kuwa majoka makengeza.
Kabla ya kustaafu babake alimchagua Jenerali Laurenco kuchukua wadhifa wa urais huku akiamini kuwa mali za familia yake hazitaguswa. Jeneral Laurenco hata hivyo ameanza kuwafurahisha Waangola kwa kuanza kumnyang'anya binti huyu baadhi ya tenda za mabilioni ya dola alizozipata wakati wa utawala wa babake. Ni kwa sababu hii net worth yake imeanza kupungua na sauti zinapazwa kuwa anafaa kutupwa jela.
Nenda katika link hii kwa habari zaidi:
Isabel dos Santos: The Fall of Africa’s Richest Woman
Aseee, Isabel nimesoma habari zake kidogo ni vile sijakariri picha yake