Mshambuliaji mahiri na nahodha wa Barcelona, Lion Mess ameendelea kuonyesha miujiza yake katika soka, baada ya jana Jumanne kufunga mabao matatu βhat-trickβ ya 48 tangu ameanza kucheza soka.
Mabao hayo aliyafunga katika mechi ya kwanza ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, yamemfanya Messi raia wa Argentina kuwa mchezaji anayeongoza barani Ulaya kwa kufunga 'hat trick' nyingi zaidi ya wengine.
Mchezaji huyo alianza kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa faulo βfree-kickβ dakika ya 31, ikiwa ni faulo ya nane kwake kufunga kwa mwaka 2018, kabla ya kukamilisha 'hat-trick' ya 42, kwa Barcelona dakika za 77 na 87, ikiwa ni ya nane kwake kwenye michuano ya Ulaya, sita alizifunga kwenye timu ya Taifa ya Argentina.
Aidha Messi ameweza kuifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Raul kwa kufunga mabao 104 katika michuano ya Ulaya akiwa ameyafunga katika michuano 14 tofauti.