Katika wale waliokuwa karibu sana na Yesu inawezekana walikuwa na mahitaji ya kutaka
watendewe miujiza lakini hawakupokea kwa sababu hawakujipambanua hata kuwa na agenda
ya kwenda nayo mbele za Yesu. Inaonekana walikazana na kuzingatia taratibu za siku zote za
mahali pale. Kuna watu walikuwa wanamfuata Yesu ili wamwone ni mtu wa namna gani au
kufuata mkumbo kutokana watu wengi kukusanyika na wengine walikuwa wakitaka kumtega ili
wamshitaki wakati wengine walitaka tena kulishwa mikate n.k. Wakati imani inapotenda kazi
na uwepo wa Mungu ukishuka, taratibu za kawaida za kibinadamu huweza huvurugika
hivyo usifungwe na mapokeo ya utaratibu wa kibinadamu (dini).
Weka mahitaji yako vizuri mbele za Mungu na kumwamini kwa moyo wote ya kuwa atatenda
kwa wakati wake, naye atafanya. Usimwendee Mungu kwa kutegemea umaarufu wa mhubiri au
kikundi fulani ili kupata mujuiza kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya na kujikuta
wakikosa majibu na hata pengine kutumbukia katika imani potofu. Siyo vibaya kwenda kwa
watumishi maarufu walioinuliwa na Mungu katika kizazi chetu lakini weka imani yako kwa
Mungu, hakikisha una agenda na hauendi kwa ushabiki au vishawishi. Ifahamu kweli ya
Mungu na iruhusu hiyo kweli ikuweke huru.