Mara nyingi mtu anapoanzisha biashara huwa na ‘mzuka’ mkubwa siku za mwanzo. Huwa anaipenda biashara yake na anawekeza nguvu nyingi huko.
Siku za kwanza biashara inapofunguliwa hata wateja huwa wengi. Sio hilo tu, hata mazingira huvutia pia. Ila, kadri siku zinavyozidi kusogea kunakuwa na uwezekano wa biashara kuyumba na hatua zisipochukuliwa mapema, hukosa uelekeo kabisa.
Hapo ndipo watu huanza kufikiria kuna mchawi anayesababisha mambo yaende kombo. Wengine wakiona biashara za watu wa karibu waliowazunguka zinashamiri, basi huwachukia wakifikiri wanawachawia.