Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Weusi wa Marekani wana tabia ya kujipa majina ya Kiafrika hasa ya Afrika Magharibi na ya Kiswahili. Kuna akina Amani, Sadiki, Nia...wengi tu....

Kuna mmoja huyu WWE naye anaitwa Nia
FB_IMG_1538778967463.jpg
FB_IMG_1538778961226.jpg
FB_IMG_1538778990737.jpg
 
Kuna baadhi ya nchi kugombea uongozi inakulazimu ufikirie mara kadhaa
Halafu unajua siri yao ni nini? Kugombea tu uongozi kwanza inabidi uwe tajiri au uwe na vyanzo vya mapato vya kueleweka. Uongozi kamwe haupaswi kuwa source ya mapato yako. Ndo maana kakosa kadogo tu unaona mtu keshajiuzulu. Siyo kama sisi huku uongozi ndiyo sehemu ya kutajirikia. Halafu eti tunaota ndoto za kutokomeza rushwa. Thubutuuu !!!
 
KATIKA ASILIMIA 100 YA WATU UNAO WAFAHAMU KUNA WANAOKUPENDA NA WASIOKUPENDA.
......
1. Asilimia 33 ya kwanza ni watu watakaokupenda wewe bila sababu yoyote.
Watu hawa watakupenda tu bila ya kujali ukoje na una nini hata kama ukipata tatizo daima watakuwa upande wako.

2. Asilimia 33 ya pili ni watu wanaokupenda wewe kwa sababu fulani mfano mali, kazi , cheo , tabia , uzuri wako n.k Tabia ya watu hawa ni kwamba upendo wao kwako unavutwa na sifa au kitu au vitu ulivyonavyo. Pia ni watu ambao kama ukiweza kuwashawishi wanaweza kukupenda sana. Lakini endapo sifa au kitu kile walichokupendea kisipokuwepo hawawezi kuwa na wewe tena mfano pesa na mali.

3. Asilimia 33 ya mwisho ni watu wasiokupenda au wanaokuchukia wewe bila ya kuwa na sababu yoyote. Watu hawa hata ufanye nini kwao huwezi kuwafurahisha zaidi ni kwamba watakuonea wivu tu na kusema kwamba unaringia mali au sifa yako. Hawa watu usiangaike nao kabisa. Zaidi ni kuwaombea tu maana hawajui walitendalo.
.....
4. Asilimia 1 iliyobaki ni wale watu ambao hawajui au hawana uhakika kama wanakupenda au wanakuchukia. Watu hawa mara nyingi ni wale wasio na msimamo kwako. Leo anaweza kuwa rafiki mzuri sana kwako lakini kesho akawa adui pia. Usiwaamini sana pia.
....
CHA KUFANYA AU CHA KUJUA HAPA NI KWAMBA SIO WATU WOTE WATAKUPENDA HATA KAMA UTAFANYA MAZURI KIASI GANI. CHA MSINGI WEWE ISHI MAISHA YAKO BILA KUMWANGALIA MTU YOYOTE KAMA ANAKUPENDA AU LAH .ILA CHA MSINGI TUNATAKIWA KUWAPENDA WOTE KWA MAANA MUNGU AMETUAGIZA TUWAPENDE WOTE HATA MAADUI ZETU TENA TUWAOMBEEE.
 
Ili tuweze kuwa na afya njema kimwili, kihisia na kiakili tunahitaji kuwa na mapumziko. Kuwa na pumziko ni mojawapo ya misingi ya kuwa na afya njema katika maisha. Sote tunahitaji kuwa na mapumziko ya kutosha kimwili , kiakili, na kihisia ili tuweze kufanya kazi zetu kwa ufanisi wa hali ya juu. Uwepo wa mapumziko ya kutosha hutusaidia katika kufanya maamuzi sahihi katika maisha yetu, kwani kukosekana huko kwa mapumziko ya kutosha kimwili, kiakili, na kihisia ndiko mara nyingi husababisha wengi kufanya maamuzi mabaya na kufikia hatua ya kujutia kutokana na kile walichokifanya.
 
Hakikisha unakuwa na mapumziko ya kutosha hata kama utakuwa umetingwa na shughuli nyingi kiasi gani. Kukosekana kwa mapumziko ya kutosha kwa wengi kumesababisha uwepo kwa athari nyingi za kiafya, migogoro na malumbano katika familia , kutokufanya kazi kwa ufanisi, na matatizo katika ndoa n.k. Na ili kuepukana na hali hizo tunahitajika kutokupuuzia hitaji la kuwa na mapumziko katika maisha yetu.
 
Wengi wetu tumekuwa tukikosa pumziko kutokana na kutingwa na shughuli mbalimbali za kimaisha pamoja na shauku zetu za kutaka kuwa juu ya wenzetu kwa kila kitu , kuwa na pesa nyingi , na hata kutaka kuwa maarufu katika kila nyanja ya maisha. Hivyo kusababisha ndoa , familia, na hata afya kupuuzwa.
 
Back
Top Bottom