Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati wakazi wa kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wamesusia kupanda vivuko vya Mv Sabasaba na Mv Ukara, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo imepiga marufuku usafiri wa mitumbwi.

Kauli hiyo imetolewa jana Jumanne Oktoba 9, 2018 katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na katibu tawala wa wilaya ya Ukerewe, Focus Majumbi.

Hata hivyo, mkutano huo ulivunjika baada ya wananchi kutokubaliana na hoja za mkuu huyo wa wilaya wakidai kuwa vivuko hivyo ni chakavu na vinaweza kuzama ama kupinduka kama ilivyotokea kwa Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, 2018 na kusababisha vifo vya watu 230.
 
Kabla ya kuvunjika kwa mkutano huo Majumbi alimtaka mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero aifute barua aliyouandikia uongozi wa vivuko hivyo akitaka visitishe huduma kwa kuwa ni chakavu.

“Ndugu zangu kilichofanyika ni kinyume na taratibu za Serikali na hatua hiyo ni sawa na uchochezi,” amesema Majumbi.

Amefafanua kuwa sheria ya vivuko inapiga marufuku uwepo wa usafiri wa mitumbwi katika eneo lenye vivuko na kutaka mitumbwi kuondolewa.
 
Baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kutoa maoni yao wamesema vivuko hivyo ni chakavu na wana hofu kuwa vinaweza kuzama, huku baadhi wakidai vimezibwa na saruji jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.

Baraka Mkondole amesema kivuko cha Mv Sabasaba kinatumia zaidi ya saa nne kwa safari moja wakati Mv Ukara kimezibwa kwa saruji, jambo alilodai ni hatari kwa maisha yao.

Majumbi alisikiliza maoni ya wananchi na kusisitiza kuwa vivuko hivyo vitaendelea kutumika kutoa huduma, jambo lililowakera wananchi hao na kuanza kumzomea.
 
Zomea zomea hiyo ilisababisha mkutano huo kuvunjika bila suluhisho kupatikana.

Kufuatia vurugu hizo, kamanda wa polisi wilaya ya Ukerewe, Ignatus Kapira aliingilia kati na kuagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani wananchi wanaotoa huduma ya usafiri kwa kutumia mitumbwi.

Kamanda Kapira amesema mtu atakayekutwa akiwashawishi wananchi kutopanda vivuko atachukuliwa hatua za kisheria.

“Ndugu zangu narudia tena asiyetaka kupanda kivuko aache lakini mkae mkijua kuwa ni marufuku kupanda mitumbwi na kuzuia wengine wanaotaka kutumia vivuko,” amesema Kapira.
 
Wakati wakazi wa kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wamesusia kupanda vivuko vya Mv Sabasaba na Mv Ukara, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo imepiga marufuku usafiri wa mitumbwi.

Kauli hiyo imetolewa jana Jumanne Oktoba 9, 2018 katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na katibu tawala wa wilaya ya Ukerewe, Focus Majumbi.

Hata hivyo, mkutano huo ulivunjika baada ya wananchi kutokubaliana na hoja za mkuu huyo wa wilaya wakidai kuwa vivuko hivyo ni chakavu na vinaweza kuzama ama kupinduka kama ilivyotokea kwa Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, 2018 na kusababisha vifo vya watu 230.
Kwahiyo kwao mitumbwi ni salama kuliko vivuko chakavu?
 
Back
Top Bottom