Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

'Lugha ya MUNGU"

Somo muhimu

Nilikumbuka nitakutafuta unielezee kiundani mkuu
Hii ni kauli ya Albert Einstein kama sikosei. Kwamba ili kuzielewa kanuni zinazoendesha malimwengu (Universes) ni lazima kwanza kuielewa lugha ambayo imetumika kuandikia kanuni hizo - Hisabati. Wakati anahangaika kuiweka nadharia yake ya Relativity sawasawa kuna wakati makalikyulesheni yalikuwa yanagoma na ilikuwa inabidi achukue muda tena kujifunza zaidi. Sir Isack Newton alikuwa mnyama katika Hisabati na alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kueleza dhana nzito nzito kisayansi kwa kanuni safi na fupi fupi za Hisabati (mf. Zile kanuni zake za mjongeo). Na baadaye akaanzisha utanzu mpya wa Kalikyulasi ambao mpaka leo na kesho sijawahi kuuelewa.

Mfano halisi unaotajwa sana kuhusu kauli hii ni yale makalikyulesheni ya John Maxwell, makalikyulesheni ambayo yaliunganisha dhana za umeme na sumaku (Electromagnetism) kwa uwazi kabisa. Wanasayansi wengi wanaamini kuwa makalikyulesheni ya huyu jamaa ndiyo mfano bora kabisa wa matumizi ya lugha ya Hisabati katika sayansi. Michio Kaku - profesa mashuhuri wa Fizikia Dhahnia huko Marekani huwa anayaitaga makalikyulesheni haya "Kazi bora kabisa ya ushairi katika Hisabati". Na magwiji karibu wote wa sayansi walikuwa pia wazuri sana katika Hisabati japo kwa viwango mbalimbali. James Watt ndiye pekee huwa anatajwa tajwa sana kuwa Hesabu zilikuwa zinampa shida.

Hii imesaidia kidogo au niendelee? Naogopa tusije tukaingia kwenye mjadala usioisha na usio na tija kama Mungu ndiye aliunda kanuni hizi zinazoendesha universe, Mungu ndiye hizi kanuni au kama kanuni hizi, kwa vile zinaeleweka na zinathibitishika, basi zinaondoa ulazima wa kuwepo kwa Mungu.
 
Dawa yake ilikuwa ni kunyoa kipara, nguo zinalowekwa kwenye maji yaliyo changanywa na dawa ya kuoshea ng'ombe (inakuwa ni mwendo wa kunuka king'ombe ng'ombe) kwa siku mbili au tatu hivi...
Uko sawa kabisa. Shida sasa ni huko vijijini unakuta vijana wa rika moja mnalala group moja hata sita au kumi. Mmoja tu akiwa nao hao jamaa basi anawagawia wote na zoezi linarudi upya. Kujikuna kichwani ngwaa ngwaaa...Na ukizubaa wanaweka makazi mpaka nguoni...
 
Wachina si ajabu wanamla huyu frog [emoji16][emoji16][emoji16]
446611104_406597.jpeg
 
Hii ni kauli ya Albert Einstein kama sikosei. Kwamba ili kuzielewa kanuni zinazoendesha malimwengu (Universes) ni lazima kwanza kuielewa lugha ambayo imetumika kuandikia kanuni hizo - Hisabati. Wakati anahangaika kuiweka nadharia yake ya Relativity sawasawa kuna wakati makalikyulesheni yalikuwa yanagoma na ilikuwa inabidi achukue muda tena kujifunza zaidi. Sir Isack Newton alikuwa mnyama katika Hisabati na alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kueleza dhana nzito nzito kisayansi kwa kanuni safi na fupi fupi za Hisabati (mf. Zile kanuni zake za mjongeo). Na baadaye akaanzisha utanzu mpya wa Kalikyulasi ambao mpaka leo na kesho sijawahi kuuelewa.

Mfano halisi unaotajwa sana kuhusu kauli hii ni yale makalikyulesheni ya John Maxwell, makalikyulesheni ambayo yaliunganisha dhana za umeme na sumaku (Electromagnetism) kwa uwazi kabisa. Wanasayansi wengi wanaamini kuwa makalikyulesheni ya huyu jamaa ndiyo mfano bora kabisa wa matumizi ya lugha ya Hisabati katika sayansi. Michio Kaku - profesa mashuhuri wa Fizikia Dhahnia huko Marekani huwa anayaitaga makalikyulesheni haya "Kazi bora kabisa ya ushairi katika Hisabati". Na magwiji karibu wote wa sayansi walikuwa pia wazuri sana katika Hisabati japo kwa viwango mbalimbali. James Watt ndiye pekee huwa anatajwa tajwa sana kuwa Hesabu zilikuwa zinampiga chenga...

Hii imesaidia kidogo au niendelee? Naogopa tusije tukaingia kwenye mjadala usioisha na usio na tija kama Mungu ndiye aliunda kanuni hizi zinazoendesha universe, Mungu ndiye hizi kanuni au kama kanuni hizi, kwa vile zinaeleweka na zinathibitishika, basi zinaondoa ulazima wa kuwepo kwa Mungu.
Duuh!! Asante mkuu
 
Back
Top Bottom