Van Dijk alisema: “Huwezi kukosa hamasa kwenye Ligi Kuu England, kwa sababu mazoezi ya kila siku ni tofauti. Kwa sababu washambuliaji wakali ni wengi, hivyo leo unafanya mazoezi ya kumdhibiti huyu, kesho unafanya mazoezi ya kumdhibiti yule.
“Cheki orodha ya washambuliaji waliopo, Eden Hazard, Sergio Aguero, Harry Kane, Olivier Giroud na wengine. Ni wazuri sana, hivyo kukabiliana nao wanakufanya uwe makini wakati wote.”Liverpool wanabanana kileleni mwa Ligi Kuu England sambamba na Manchester City na Van Dijk amekuwa mtu muhimu.