Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UNAAMBIWA hivi, usikate tamaa kwa chochote unachokifanya kwa chochote unachopitia. Changamoto ni sehemu ya kuishi, hivyo unapaswa kupambana nalo na ushahidi wa hilo upo kwa wanasoka hawa ambao maisha yao yalikuwa magumu sana utotoni kabla ya sasa kuishi kibosi.
 
Cristiano Ronaldo

Supastaa wa Juventus ndivyo anavyotambulika kwa sasa. Lakini, asikwambie mtu, Cristiano kama angekuwa lelemama utotoni, asingefika hapo alipo kwa sasa, akiwa mwanasoka tajiri mkubwa na kuishi maisha anayochagua yeye. Ronaldo amekulia katika maisha ya kimasikini sana, wazazi wake hawakuwa na kazi zenye kipato kikubwa kiasi cha kumfanya utoto awe analala chumba kimoja na ndugu zake wanne, akiwamo dada zake wawili.
 
Alianzia soka mtaani, kabla ya kufanya majaribio Sporting CP na kufuzu. Akamwomba mama yake aache shule, akakubalika, kipaji chake kikampa dili tamu Manchester United, Real Madrid na sasa Juventus huku akishinda tuzo ya Ballon d’Or mara tano.
 
Neymar

Huduma yake ndio ghali zaidi kwa sasa. Saini yake iliwafanya PSG kuilipia Pauni 198 milioni kumnasa kutoka Barcelona mwaka jana. Lakini, Neymar ana stori yake inayosikitisha na kuhamasisha. Akiwa na umri wa miezi minne tu ya kuzaliwa kwake, Neymar alipata ajali ya gari na hali yake ilikuwa mbaya. Familia yake walidhani wanampoteza mtoto wao, lakini mambo yalikuwa sawa na Neymar akawa kwenye afya timamu. Familia yake iliishi kwenye chumba kimoja chakavu hadi hapo Neymar alipoanza kupata pesa zilizotokana na malipo yake ya kucheza mpira na kuwanunulia nyumba wazazi wake. Uchu wa kufikia mafanikio makubwa kwenye kile anachokifanya ndicho kilichomfanya Neymar kuwa hapo alipo kwa sasa akimiliki aina zote za usafiri, magari, ndege hadi boti.
 
Zlatan Ibrahimovic

Staa Zlatan Ibrahimovic wazazi wake walitengana wakati ana umri wa miaka miwili tu. Baada ya hapo, maisha hayawahi kuwa rahisi kwa Zlatan, ambapo utoto wake ulikuwa na mapito mengi ikiwamo wizi. Aliwahi kukiri kwamba aliwahi kuiba baiskeli ili imsaidie kufika mazoezini. Soka ndicho kitu kilichokuwa kikimpa matumaini kwamba kuna siku atafikia malengo anayotaka na ndipo alipopambana hadi hapo alipobamba nafasi ya kuitumikia klabu ya Malmo FF ya huko kwao Sweden kabla ya kupita kwenye klabu nyingi kubwa za Ulaya na sasa kuwa mmoja wa wanasoka matajiri duniani.
 
Franck Ribery

Maisha ya utoto aliyokuwa akiishi supastaa wa Bayern Munich, Franck Ribery hayalingani kabisa na haya ya sasa. Kwa sasa staa huyo anamiliki anachokitaka kutokana na pesa yake anayovuna kila wiki kwenye ujira wake huko Allianz Arena. Lakini, huko utotoni familia ya staa huyo haikuwa na kipato kikubwa sana kiasi cha kumfanya Ribery mara kadhaa aungane na baba yake kwenda kufanya kazi za ujenzi. Mwenyewe anafichua kwamba jambo hilo lilimpa funzo kubwa sana katika maisha yake.
 
Luis Suarez

Mashabiki wa Real Madrid viroho vinalipuka linapotajwa jina la Luis Suarez. Hata wiki bado haijapita, tangu alipowapiga tatu kwenye El Clasico, ambapo Los Blancos walikubali kipigo cha 5-1 huko Nou Camp. Suarez wa sasa huwezi kushangaa kusikia yupo kwenye viwanja vya gharama kubwa akifanya starehe na familia yake, kwa sababu pesa anayo kutokana na ujira wake anaolipwa na Barcelona. Lakini, utoto mambo yalikuwa tofauti. Suarez alitelekezwa na baba yake akiwa na miaka 12 na kipindi hicho alikuwa akicheza mpira pekupeku. Ilibidi aishi kwa shida sana ikiwa pamoja na kufanyakazi za kufagia barabarani kupata pesa. Lakini, sasa Suarez ni mtu huko Barcelona.
 
Alexis Sanchez

Alexis Sanchez alipofika Ulaya alitamba kwenye klabu za Udinese, Barcelona, Arsenal na sasa yupo Manchester United anakolipwa mshahara wa kibosi. Pochi yake kwa sasa imetuna kutokana na mshahara anaolipwa huko Old Trafford, Pauni 500,000 kwa wiki. Lakini, utotoni kwake, Sanchez maisha hayakuwa rahisi. Mama yake alikuwa akifanya kazi ya ufagiri kwenye shule moja hivi, huku yeye mwenyewe alifanya sana kazi za kuosha magari kuongeza kipato nyumbani. Hata mpira wenyewe aliokuwa akicheza mwanzoni hakuwa na viatu hapo hapo alipopata msaada ya kufadhiliwa na mtu jozi zake za kwanza za viatu vya kuchezea soka.
 
Luka Modric

Ndiye mwanasoka bora wa Ulaya kwa sasa. Amebeba tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora huko Russia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 akiwa na kikosi chake cha Croatia. Lakini, maisha ya kiungo huyo fundi wa mpira wa Real Madrid akiwa na umri wa miaka mitano tu, nchi yake ilikuwa na vita kali na mji aliokuwa akiishi ulikuwa umetekwa. Jambo hilo lilimwaathiri sana mchezaji huyo akiwa mtoto kabla ya kuendeleza kipaji chake cha soka baada ya hali ya usalama kutengemaa na Modric akiennda kutamba Tottenham Hotspur kabla ya sasa kukipiga kwenye kikosi cha Los Blancos.
 
Angel Di Maria

Matatizo ya kiafya yalitishia kipaji chake cha soka lakini maisha ya soka yalizidi kuendelea na kukua pamoja nae. Ilikuwa ngumu kwa familia yake iliyokuwa na watoto watatu pamoja na baba na mama kutimiza mahitaji muhimu hivyo ilimlazimu Di Maria aungane na dada zake pamoja baba yake ili kufanya kazi katika makaa ya mawe. Kipaji cha soka kilimfanya Di Maria anaswe na Rosario Central na baadaye Benfica, ambayo ndiyo iliyomaliza matatizo ya familia hiyo kabla ya winga huyo kutimkia Real Madrid, Manchester United na sasa anatamba na Paris Saint-Germain.
 
Yaya Toure

Kiungo, Yaya Toure kwa sasa anakipiga Olympiacos baada ya mkataba wake kufika tamati huko Manchester City. Lakini, Muivory Coast huyo aliwahi kuitumikia pia Barcelona. Hata hivyo, hayo ni mambo ya baadaye sana, huko utotoni Yaya alikuwa na maisha magumu, akicheza soka bila ya viatu. Kina Yaya kwenye familia yao walikuwa wengi, hivyo chakula ndicho kilichokuwa kitu muhimu na si kununua viatu vya kuchezea mpira. Baadaye sana, Yaya ndio alianza kuchezea viatu, lakini huko nyuma mwendo ulikuwa ni kucheza soka pekupeku.
 
Wachezaji wengine

Orodha ya wachezaji ambao waliishi maisha magumu utotoni kabla ya sasa kuishi kibosi ni pamoja na Yuri Zhirkov, Robinho, Antonio Cassano, Samuel Eto’o, Carlos Tevez, Wayne Rooney, Dani Alves, Alex Hleb na Mbrazili, Dante ambao walikumbana na changamoto nyingi wakati wanakuwa kabla ya sasa kupambana na kuwa wanasoka maarufu na wenye pesa nyingi wakinunua kitu wanachotaka tofauti na walikotokea, ilikuwa wanakula kilichopo na si wanachokitaka.
 
FB_IMG_1541074789684.jpg
 
Back
Top Bottom