Kwa maana hiyo, Ramsey sasa atakuwa huru kuachana na Arsenal bure kabisa mwishoni mwa msimu huu kwa sababu klabu yake haina mpango wa kumpa mkataba mpya.
Ramsey alilalamika wiki iliyopita kwamba amekuwa haelezwi mwenyewe bayana kitu kinachoendelea kuhusu mkataba mpya baada ya Arsenal kuondoa ofa yao, lakini sasa amewekwa wazi kwamba mkataba wake wa sasa ukifika tamati tu mwisho wa msimu, basi ashike njia zake. Mabosi wa Arsenal wanadai kwamba kwa sasa wanachozingatia ni afya ya kipesa ya timu na ndio maana hawawezi kufanya kile Ramsey anachotaka kifanywe kwenye mipango ya mkataba wake mpya. Arsenal wameshajiandaa kwamba kama hakutakuwa na timu itakayotaka kumsajili kwenye dirisha la Januari basi itamwaachia bure kabisa mwisho wa msimu.