Juninho
Baada ya kuisaidia Brazil kutwaa Kombe la Dunia, mwaka 2002 Korea Kusini, ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa, Antonio Augusto Ribeiro Reis Junior, maarufu kama Juninho Pernambucano, angejiunga na Middlesbrough.
Yaani katika klabu zote vilivyokuwa vinamtolea macho, moyo wake ukamtuma kwenda Riverside, Kaskazini mwa Mji wa Yorkshire, Uingereza kujiunga na Teesiders, Dunia ina mambo kweli.
Mwaka 2004, aliisaidia klabu hii kutwaa ubingwa taji lake la kwanza ilipotwaa Kombe la Ligi, na kufuzu Michuano ya Kombe la Uropa, kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.