Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Arsenal haikushawishi sana mechi yake iliyopita dhidi ya Bournemouth lakini ilichukua pointi tatu na mshambuliaji wake, Pierre-Emerick Aubameyang ni mtu ambaye yupo katika fomu na ni mmoja kati ya washambuliaji hatari katika ligi.
 
Wakati Owen akidai hivyo, staa wa zamani wa Arsenal na Timu ya Taifa ya England, Paul Merson ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka England naye alishikwa na kigugumizi cha kutabiri matokeo ya pambano hilo ingawa alidai Arsenal ndio ipo katika presha ya kushinda mechi hiyo kuliko Tottenham.
 
Mechi hii ya wikiendi hii ni kubwa kwa Arsenal kuliko kwa Tottenham. Hivyo ndivyo ilivyo. Kama Tottenham ikicheza kama ilivyocheza dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita haiwezi kupoteza. Lakini imecheza vizuri zaidi mechi hiyo tu na haijawa vizuri sana bado pamoja na kuanza msimu vizuri,” alisema Merson.
 
Kuelekea pambano hilo, mashabiki wa Arsenal wamekuwa na wasiwasi na uteuzi wa mwamuzi wa pambano hilo, Mike Dean ambaye wanaamini ana unazi fulani na wapinzani wao, Tottenham kutokana na kashfa kadhaa pindi anapochezesha mechi za wapinzani hao.
 
Dean alishutumiwa kushangilia bao la Spurs katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa msimu wa 2015/16 lakini vilevile inadaiwa alimruhusu kiungo, Mousa Dembele kufunga licha ya kumchezea madhambi beki wa Villa, Ciaran Clark.
 
Mwaka 2012 mashabiki wa Arsenal walimshutumu mwamuzi huyo wa kushangilia bao la Tottenham lililofungwa na mshambuliaji, Louis Saha katika pambano dhidi yao ingawa katika pambano hilo Arsenal iliondoka na ushindi mnono wa 5-2.
 
Rais wa zamani wa Marekani George H W Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94, mwanawe rais wa zamani pia George W Bush ametangaza.
George Bush Senior, kama alivyofahamika sana, alifariki dunia mwendo wa saa nne na dakika kumi usiku (saa kumi na dakika kumi GMT), msemaji wa familia hiyo ametangaza.
Alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1993 baada ya kuongoza kwa mihula miwili kama makamu wa rais chini ya Rais Ronald Reagan.
 
Aprili, alilazwa hospitalini akiwa na maambukizi kwenye damu lakiniakatibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
George Herbert Walker Bush amefariki miezi saba tu baada ya kifuo cha mke wake Barbara.
Viongozi wamekuwa wakituma salamu za rambirambi na kumkumbuka mwanasiasa huyo, wakiongozwa na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump aliyemsifu kwa "uhalisiwa wake, ucheshi na kujitolea kwake kudumisha imani, kwa familia na kwa taifa.
Bendera katika ikulu ya White House zitapepea nusu mlingoti huku mipango ya mazishi ikiendelea.
 
George H W Bush alikuwa mtu wa aina gani?
Kuapishwa kwa George H W Bush kuwa Rais wa Marekani mnamo Januari 1989 kilikuwa kilele cha ufanisi wake katika siasa. Alikuwa ameandiliwa kwa muda mrefu kupitia mafunzo ya kiwango cha juu, na kupandishwa madaraka mara kwa mara kabla ya kuishia Ikulu ya White House.
Rais huyu wa 41 wa Marekani alifanya kazi kama makamu wa Rais wa Ronald Reagan kwa miaka minane.
 
Alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza aliyekuwa afisini kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais katika kipindi cha zaidi ya miaka 150.
Utawala wake unahusishwa sana na siasa za wakati ule ambapo Ukomunisti ulikuwa ukiporomoka Ulaya Mashariki na kusambaratika kwa Muungano wa Usovieti (USSR) ambapo Marekani iliachwa ikiwa taifa kubwa zaidi kiuchumi na kiviwanda duniani.
Uongozi wake ulisaidia kurejesha hadhi ya Marekani kwa dunia nzima na kurejesha heshima yake kufuatia uvamizi wa Marekani nchini Vietnam, ulioiletea Marekani aibu.
 
Hata hivyo alilaumiwa kwa kupuuza maswala ya ndani ya Marekani na kwa kupuuzilia mbali ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni ambapo aliahidi kuwa hataongeza kodi.
Kupuuzilia mbali kwa ahadi hiyo kulimfanya ashindwe katika uchaguzi uliofuata na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1992.
 
Maisha ya kisiasa
1966: Alishinda kiti katika Bunge la Wawakilishi
1971: Nixon amteua kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
1974: Ateuliwa kuwa Balozi wa Marekani katika ubalozi mpya nchini Uchina
1976: Ford amteua kuwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la CIA
1981-1989: Makamu wa Rais wa Ronald Reagan
1989-1993: Rais wa Marekani; aongoza Marekani katika Vita vya Kwanza vya Ghuba; akabiliana na hali ya kuporomoka kwa Ukomunisti Ulaya Mashariki.
 
May His Soul Rest In Peace.
 
George Herbert Walker Bush alizaliwa Julai 12, 1924 katika Milton, Massachusetts. Baba yake alikuwa mwekezaji katika benki na baadaye akawa Seneta wa Marekani.
Alijitolea kupigana katika jeshi la wanamaji Vita Vikuu vya Pili vya Dunia baada ya kushambuliwa kwa Pearl Harbor. Alipata mafunzo ya kuendesha ndege za kivita kabla ya kupewa majukumu katika vita katika Bahari ya Pacific ambapo alishiriki katika vita dhidi ya Wajapani katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
 
Akiwa na umri wa miaka 18 pekee, ambapo inawezekana alikuwa miongoni mwa marubani wachanga sana Wamarekani, alipewa kazi ya urubani wa ndege za kijeshi za kuangusha mabomu zinazoruka angani kutoka kwa meli kubwa za kivita.
Ndege yake ilitunguliwa Septemba 1944 alipokuwa akielekea kuangusha mabomu. Ndege yake ilijaa moshi na ndimi za moto zilianza kuteketeza mbawa zote mbili. Anakumbuka akisema: "Mungu wangu! Ndege hii italipuka.''
 
Aliendelea kuendesha ndege hiyo na kuangushia mabomu shabaha zake kadhaa. Aliwaamuru wanahewa wawili aliokuwa nao wajisalimishe kwa kuruka kwa miavuli kutoka kwenye ndege hiyo lakini wote wawili hawakunusurika.
Bush alisongwa na moshi lakini akavalia mwavuli pia na kuruka kama wenzake. Alianguka kwenye kisiwa kimoja baada ya kugongwa kichwa chake na sehemu ya nyuma ya ndege kwa sababu ya upepo akiruka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…