Kwa Madrid, kama ilivyo kwa United, inamwania Pochettino, 46, ikiamini ni kocha kijana, mwenye nguvu, ambaye ana kiu ya ushindani.
Bosi Mtendaji wa United, Ed Woodward inadaiwa alipendelea Mourinho aendelee mpaka mwishoni mwa msimu lakini baada ya kichapo cha Jumapili cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool huku United ikaondoka na takwimu mbovu uwanjani yeye na wenzake waliamini imetosha.