Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Liverpool ilimnasa Salah kwa ada ya Pauni 36 milioni na alipotua tu kwenye kikosi hicho cha Anfield amefanya mambo makubwa ikiwamo kufunga mabao 44 katika mechi 52 alizocheza kwenye timu hiyo huku akishinda Tuzo ya Bao Bora la Mwaka kupitia lile aliloifunga Everton.
 
THE Special One amefikia mwisho Manchester United na sasa ukomo huo huko Old Trafford umepachikwa jina la The Special End.

Kocha Jose Mourinho alifunguliwa mlango wa kutokea Old Trafford juzi Jumanne asubuhi na jambo hilo limehitimisha miezi yake 31 aliyokuwa kwenye kikosi hicho cha Man United.
 
Kufukuzwa kazi si kitu kipya kwa kocha huyo kwani jambo hilo lilimtokea Chelsea mara mbili na pia alifutwa kazi pia alipokuwa na wababe wa Bernabeu, Real Madrid.

Hata hivyo, safari hii kibarua chake kimeota nyasi huko Old Trafford vizuri kwani ataweka kibindoni Pauni 24 milioni kama fidia kutokana na mkataba wake kuvunjwa.
 
2016

Mei 27 - Baada ya miezi kadhaa ya fununufununu, hatimaye Man United ilimteua Mourinho kuwa kocha wake, akichukua mikoba ya Louis van Gaal kama kocha wa kudumu huko Old Trafford.

Juni/Julai - Afanya usajili kwa kuwanasa Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan kujiunga na Man United.

Julai 6 - Mourinho aamua kuishi tu hotelini, kwenye Hoteli ya Lowry na alibaki hapo hadi anafukuzwa kazi.

Agosti 7 - Mourinho ashinda Ngao ya Jamii.

Agosti 9 - Mourinho amsajili Paul Pogba kwa Pauni 89 milioni.

Septemba 11 - Afungwa na Pep Guardiola katika mechi ya kwanza ya Manchester derby.

Oktoba 27 - Mourinho apigwa faini ya Pauni 50,000 na kufungiwa mechi moja baada ya kumkosoa Mwamuzi Anthony Taylor

Novemba 6 - Awashambulia mabeki wake Chris Smalling na Luke Shaw kwa kukataa kucheza dhidi ya Swansea City, ambapo wachezaji hao walisema wao ni majeruhi, lakini Mourinho alitaka wajikaze na kucheza hivyo hivyo na majeraha yao.

Novemba 28 - Aondoshwa tena kwenye benchi lake na kutakiwa akakaye jukwaani baada ya kupiga teke chupa ya maji kwenye mechi dhidi ya West Ham United.
 
2017

Februari 26 - Mourinho ashinda Kombe la Ligi, akiwa kocha wa kwanza wa Man United kushinda taji hilo msimu wa kwanza.

Mei 24 - Ashinda taji la Europa League baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ajax.

Julai - Mourinho asajili Victor Lindelof, Romelu Lukaku na Nemanja Matic.

Septemba 8 - Mourinho amkosoa Andreas Pereira kwa uamuzi wake wa kwenda kwa mkopo badala ya kubaki kwenye timu na kugombea nafasi kikosini.

Septemba 10 - Mourinho alumbana na Mark Hughes wakati wa mechi na hivyo wakashindwa kupeana mikono mechi ilipomalizika.

Oktoba - Mourinho achukia kisa Pogba kusafiri kwenda Miami, Marekani kutibu misuli.

Desemba 11 - Mourinho ahusika kwenye malumbano na kipa wa Man City, Ederson huko kwenye vyumba vya kubadilishia na kumfanya kocha huyo kurushiwa chupa ya maziwa na maji.

Desemba 26 - Mourinho alilalamika matumizi yake ya Pauni 300 milioni kunasa wachezaji wapya haikutosha kwa sababu Man City imetumia pesa nyingi kununua mabeki wa pembeni kwa bei ya kusajili mastraika.
 
2018

Januari 5 - Vita ya maneno yaendelea baina yake na Antonio Conte, Mourinho akisema kamwe haitatokea siku akakumbwa na kashfa ya kupanga matokeo.

Januari 22 - Mourinho amchukua Alexis Sanchez kutoka Arsenal na kumlipa Pauni 300,000 kwa wiki baada ya makato, huku akimtoa Henrikh Mkhitaryan kwenda Arsenal.

Januari 25 - Mourinho asaini mkataba mpya Man United unaomfanya kuwa Old Trafford hadi Juni 2020.

Januari 31 - Pogba atolewa kwenye mechi dhidi ya Tottenham baada ya kulumbana na kocha hadharani.

Aprili 7 - Pogba afunga mara mbili Man United ikitoka nyuma kuwafunga mahasimu wao Man City 3-2, wakiwazuia kutangaza ubingwa.

Aprili 27 - Mourinho akadai anajuta kutokana na kulumbana kwa muda mrefu na Kocha Arsene Wenger.

Mei - Man United yamaliza msimu wa Ligi Kuu England ikiwa nafasi ya pili.

Mei 12 - Msaidizi wa miaka mingi wa Mourinho, Rui Faria atangaza kuachana na kocha huyo na badala yake Mourinho anamtangaza Michael Carrick kuwa msaidizia wake.

Julai 1-3 - Man United yawasajili Diogo Dalot, Fred na kipa wa kikosi cha akiba huko Stoke City, Lee Grant.

Julai 24 - Baada ya Pogba kutwaa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa, Mourinho alimpiga kijembe mchezaji wake huyo badala ya kumpongeza
 
Julai 28 - Mourinho alalamikia kuhusu usajili, akisema: “Nimempa bosi orodha ya wachezaji watano ninaowataka miezi michache iliyopita na nilikuwa nikisubiri kuona kama kuna hata mmoja atakuja.”

Agosti 10 - Baada ya ushindi dhidi ya Leicester City, Pogba alisema: “Kama huna furaha, huwezi kujitolea kwa kiwango cha ubora wako.”

Agosti 16 - Ugomvi mkubwa umetokea, Mourinho amwambia Pogba kama anataka kuondoka basi aandike barua ya kuomba kuuzwa.

Septemba 23-24 - Pogba amkosoa Mourinho mbinu zake baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Wolves, akisema Man United inapaswa kucheza soka la kushambulia.
 
Agosti 16 - Ugomvi mkubwa umetokea, Mourinho amwambia Pogba kama anataka kuondoka basi aandike barua ya kuomba kuuzwa.

Septemba 23-24 - Pogba amkosoa Mourinho mbinu zake baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Wolves, akisema Man United inapaswa kucheza soka la kushambulia.

Septemba 25 - Baada ya kumvua unahodha msaidizi, Mourinho aliamua kumpiga kijembe Pogba kwenye mipango yake. Lakini, Pogba alilichukulia hilo kawaida tu.

Septemba 26 - Ugomvi waibuka, Pogba akimweleza hana adabu, tukio hilo lilinaswa na kamera za waandishi wa habari.
 
Septemba 29 - Pogba aliwaambia waandishi wa habari, ‘Mnataka nife?’

Baada ya Man United kukumbana na kipigo cha 3-1 kutoka kwa West Ham. Siku chache baadaye, alisema amekuwa akisakamwa.

Oktoba 16 - Mourinho akumbana na adhabu ya FA baada ya kufanya kitu kisichoruhusiwa mbele ya kamera baada ya kuifunga Newcastle United.

Novemba 27 - Mourinho aliwashangaza watu uwanjani Old Trafford baada ya kuchukua chupa za maji na kuzipigisha chini baada ya kiungo Marouane Fellaini kufunga bao la ushindi dhidi ya Young Boys kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Desemba Mosi - Pogba aambiwa yeye ni kirusi na kocha Mourinho baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Southampton.

Kiungo huyo wa Ufaransa amekataa kubebeshwa lawama akisema hahusiki na matatizo yanayoendelea kwenye timu hasa kwa upande wa timu kuboronga.

Desemba 7 - Wakala maarufu Mino Raiola, ambaye aliripotiwa kuzungumza na Barcelona na Juventus kwa ajili ya mteja wake, Pogba, amewaambia Man United, mteja wake anataka alipwa mshahara wa Pauni 200,000 baada ya makato ya kodi ili aendelee kubaki Old Trafford.
 
Desemba 8 - Romelu Lukaku, anayesimamiwa pia na wakala Mino Raiola, amekuwa staa mwingine wa Man United kutaka kuihama timu hiyo kisa Kocha Mourinho.

Desemba 12 - Mourinho alisema hakuwa akivutiwa na Pogba na baadhi ya wachezaji wengine baada ya kuonekana kucheza hovyo kwenye mechi ya kipigo dhidi ya Valencia.

Desemba 16 - Pogba awekwa kando kikosini kwenye mechi dhidi ya Liverpool.

Hakucheza kabisa na timu ikachapwa kwenye mechi hiyo na kuachwa pointi 19 na mahasimu wao hao wakubwa.

Desemba 18 - Mourinho afukuzwa, atalipwa Pauni 24 milioni fidia ya kuvunja mkataba wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…