Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KOCHA wa Chelsea, Maurizio Sarri amewataka mabosi wake kufanya haraka kumalizana na staa wake Eden Hazard ili kumaliza tatizo hilo. Sarri alisema, Chelsea ni lazima wamalize tatizo hilo baada ya Hazard kuonekana kugomea kusaini dili jipya, huku mkataba wake wa sasa ukitarajia kumalizika 2020 na Real Madrid wanamtolea macho Mbelgiji huyo.
 
Hazard ameamua kusubiri hadi mwisho wa msimu ndipo atakapoamua kuhusu dili la muda mrefu la kuendelea kubaki kwenye timu hiyo ya Stamford Bridge. Sarri alipoulizwa kuhusu Hazard juu ya msimamo wake kwenye kikosi cha Stamford Bridge akisema mabosi wake wanapaswa kukamilisha dili hilo mapema ili ifahamike wazi mbivu na mbichi. Hazard anasumbua kwa sasa juu ya msimamo wake huo huku Real Madrid wakionekana kuwa ndio chanzo kwa sababu wameonyesha dhamira ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo na wanasubiri ifike mwisho wa msimu kwa sababu hapo Mbelgiji huyo atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, hivyo atapatikana kwa bei yenye unafuu mkubwa.
 
Christian Pulisic
LIVERPOOL imeripotiwa kwamba ipo karibu kabisa kuwapiku Arsenal na Chelsea kwenye mbio za kumnasa supastaa wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic. Liverpool wamekoleza mwendo wao katika kuinasa huduma ya mchezaji huyo baada ya Bayern Munich kujiweka kando katika kumfukuzia winga huyo. Lakini, Chelsea wanamtaka kwa nguvu zote.
 
Gonzalo Higuain
MKURUGENZI wa michezo wa AC Milan, Leonardo amesema kwamba hakuna ofa yoyote waliyopokea kutoka Chelsea kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji, Gonzalo Higuain. Chelsea walionyesha nia ya kumsajili Higuain tangu kwenye dirisha la majira la kiangazi mwaka huu, lakini Muargentina huyo aliamua kwenda zake AC Milan kwa mkopo akitokea Juventus.
 
Abdoulaye Doucoure
KOCHA wa Watford, Javi Garcia amesema kwamba amekuwa na matumaini makubwa ya kumbakiza kiungo Abdoulaye Doucoure kwenye kikosi chake. Staa huyo wa Ufaransa amekuwa akiwinfwa na PSG na huenda akanaswa kwenye dirisha la Januari ili kwenda kuchukua nafasi ya Adrien Rabiot. Lakini, kocha Garcia anaamini mabosi wake watambakiza Doucoure kikosini.
 
Cesc Fabregas
CHELSEA inafanya mipango ya kuachana na kiungo wake Cesc Fabregas ili akajiunge na timu yoyote anayotaka kwa uhamisho wa bure kabisa bila ya senti hata moja. Ripoti zinadai kwamba Fabregas anataka yupo kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba wake kabla ya mwisho wa msimu kufika ili akajiunge timu nyingine itakayompa muda wa kucheza. Monaco inamtaka sana.
 
Ever Banega
STAA wa Sevilla, Ever Banega ameamua kubadili wakala ili kuhakikisha anakamilisha ndoto zake za kuhamia England. Ripoti zinadai kwamba Banega ameona kubadili wakala kutatimiza mpango wake huo wa kutua kwenye Ligi Kuu England. Staa huyo wa Argentina anataka kwenda kujiunga na Arsenal inayonolewa na kocha wake wa zamani, Unai Emery.
 
Luka Modric
KIUNGO, Luka Modric ameripotiwa kwamba amegoma kusaini mkataba mpya huko Real Madrid ikiwa ni mipango yake ya kutaka kuachana na timu hiyo. Modric ni mmoja wa wachezaji wanaotaka kuachana na timu hiyo ambayo mambo yamekuwa magumu tangu kuondoka kwa kocha Zinedine Zidane. Mkataba wake wa sasa unafika tamati 2020.
 
Wilfried Zaha
KOCHA, Roy Hodgson amezipuuza na kuziona za kijinga kabisa tetesi za kwamba staa wake huko Crystal Palace, Wilfried Zaha kwamba atashawishika na mpango wa kuihama timu hiyo na kutimkia China. Klabu ya China, Dalian Yifang imeripotiwa kumtaka Zaha na kwamba imemwaandalia mshahara wa Pauni 11 milioni kwa mwaka ili akacheze China.
 
Wilfried Zaha
KOCHA, Roy Hodgson amezipuuza na kuziona za kijinga kabisa tetesi za kwamba staa wake huko Crystal Palace, Wilfried Zaha kwamba atashawishika na mpango wa kuihama timu hiyo na kutimkia China. Klabu ya China, Dalian Yifang imeripotiwa kumtaka Zaha na kwamba imemwaandalia mshahara wa Pauni 11 milioni kwa mwaka ili akacheze China.
 
Rob Elliot
NEWCASTLE United imeripotiwa kukaribisha ofa kutoka kwa timu mbalimbali zinazovutiwa na kipa Rob Elliot. Kocha Rafa Benitez alisema kwamba kipa huyo kwa sasa anapatikana tu kwa timu yoyote inayomhitaji kwa sababu kwenye kikosi chake kuna makipa Martin Dubravka, Freddie Woodman na Karl Darlow wote hao ni mahiri na wanamzidi Elliot.
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…