Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MWAKA mpya umefika tena na dirisha dogo la usajili litashuhudia wachezaji kadhaa wakihama klabu zao kwenda ambako tetesi zimekuwa zikielekezwa, japo kuna uwezekano wa mabadiliko kutokana na matukio kadhaa.
 
Iwe wanafukuzia ubingwa au kombe jingine, kuwania kupanda daraja au kuepuka kushuka, makocha watakuwa wanatarajia viongozi wa klabu zao kutoa vitabu vya hundi na kuwaandikia klabu nyingine ili wanunue wachezaji wanaowataka kuleta. Majina makubwa ambayo yalikuwa yakitajwa na kuhusishwa na kuhama katika dirisha hili la Januari ni pamoja na akina Paul Pogba, Isco na Adrien Rabiot. Paul Pogba (25) ambaye ni kiungo wa Manchester United alihusishwa kuhamia ama Juventus alikotokea kabla, Barcelona au Paris St-Germain ambao ni ya kwao Ufaransa.
 
Hili ndilo jina kubwa zaidi kwenye orodha yetu, ambapo aliponunuliwa na Man United alishikilia rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani, akinunuliwa na Jose Mourinho kwa pauni milioni 89. Moja ya sababu kubwa za kuondoka ni uhusiano mbovu baina yake na Mourinho ambaye hata hivyo ameshafukuzwa Old Trafford baada ya timu kufanya vibaya.
 
Kuondoka kwa Mourinho kunaweza kusababisha akabaki japokuwa bado kuna taarifa za kaandaliwa dau kubwa la Pauni 125 milioni kumnasa, Barca na PSG wakitajwa zaidi kumtaka. Haijulikani ikiwa atataka kuondoka au atabaki hapo ambako kumepoa baada ya ‘mbaya’ wake kuondoshwa.
 
Kuna kiungo aliyehamia Chelsea ambaye sasa ana umri wa miaka 28 naye ni Danny Drinkwater aliyepata kutwaa ubingwa akiwa na Leicester. Huyu mambo yake hayajakwenda yalivyotarajiwa hapo Stamford Bridge na amekuwa akihusishwa kwenda ama West Ham au Fulham. Mechi pekee aliyocheza msimu huu ni kwenye Ngao ya Jamii waliyopoteza mbele ya Manchester City na sasa ameambiwa na kocha, Maurizio Sarri kwamba anaweza kuondoka Januari hii. Upo uwezekano, kwa hiyo, wa kuungana na bosi wake wa zamani Claudio Ranieri ambaye sasa yupo Fulham.
 
Tukibaki Chelsea tunamwona mchezaji wao mkongwe Garry Cahili mwenye umri wa miaka 33 na mahiri kwenye ulinzi ambaye anahusishwa na Arsenal, AC Milan, Aston Villa na Fulham. Huyu kwa hakika ni mwingine asiyependwa Chelsea na bosi Sarri kiasi cha kushindwa kuingia kikosi cha kwanza cha bosi huyu Mtaliano na ameshaambiwa anaweza kuondoka. Kutokana na uzoefu wake katika Ligi Kuu ya England (EPL) lakini pia kimataifa, ni wazi Cahil ana nafasi kubwa ya kuitwa na klabu za ndani au nje ya nchi.
 
Zipo taarifa pia kwamba Bayern Munich wanavamia Chelsea wakitaka kumchukua tineja wao, Callum Hudson-Odoi anayeibukia wakati mchezaji mwenzake, Cesc Fabregas aliyelia sana baada ya mechi ya Kombe la FA dhidi ya Nottingham Forest, ameaga na kutimukia AS Monaco. Anakwenda kujiunga na mchezaji mwenzie wa zamani, Thierry Henry klabuni Monaco. Wengine wanaodhaniwa kupewa kwa heri Stamford Bridge ni Victor Moses na Andreas Christensen ambao wanaonekana wazi kwamba hawapo kwenye mipango ya mwalimu Sarri.
 
Brahim Diaz ni kijana mwenye umri wa miaka 19 akiwa kiungo wa klabu ya Manchester City ambaye mkataba wake unamalizika, akiwa anachanganyikiwa kwa kukosa muda wa kutosha wa kucheza na akikosa fursa za kikosi cha kwanza. Ikumbukwe huyu ni mchezaji wa kimataifa (U-21) wa Timu ya Taifa ya Hispania na angependa kuwika zaidi ili apande kwenye timu ya wakubwa. Zipo taarifa kwamba atajiunga na Real Madrid kwa pauni milioni 13.6 kwenye dili atakalopata mshahara wa pauni 60,000 kwa wiki.
 
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England, Jermain Defoe (36) anafikiriwa kwamba ataondoka Bournemouth na anahusishwa kujiunga na moja ya klabu kati ya Crystal Palace, Nottingham Forest, Sheffield United naWigan umri ukiwa unasonga, Defoe amekuwa na wakati mgumu msimu huu, akicheza pungufu ya dakika 30 kwenye mechi za EPL. Lakini huyu ni mchezaji anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga mabao mengi zaidi (162) muda wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…