Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tofauti na samaki ambao huendeleza vizazi vyao kwa kutaga, nyangumi si samaki bali ni mnyama anayeishi baharini, ingawa umbo lake hufanana na samaki mkubwa hususani kichwa, baadhi ya sehemu za mwili na mkia, lakini hayo hayaondoi sifa yake ya kuitwa mnyama kwani ni kiumbe anayezaa na kunyonyesha, jike huwa na matiti mawili ambayo humsaidia kumpatia ndama wake chakula kwa kumnyonyesha, hubeba mimba kwa miezi 12 na huzaa mtoto mmoja tuu, ambapo anapozaliwa hutanguliza mkia ili kuzuia kifo kinachoweza tokana na kukosa hewa, na punde baada ya kuzaliwa tuu mtoto huyo huanza kuogelea kuelekea juu ya uso wa bahari kwa msaada wa mama yake ili akapate hewa, ndama wa nyangumi hunyonya takribani lita 250 mpaka 400 za maziwa kutoka kwa mama yake kila siku, mpaka hapo atapotimiza mwaka mmoja.
 
Mtoto wa nyangumi atimazapo mwaka mmoja humuacha mama yake na kuanza kujifunza mbinu za kujitegemea, pamoja kwamba huendelea kukaa jilani na mama yake, ndama hao hupevuka watimizapo miaka saba mpaka kumi, kwa umri nyangumi huishi miaka mingi hufikia miaka 80 mpaka 90 na wapo jamii nyingine ya nyangumi ambao hufikisha miaka zaidi ya 100.
 
Urefu wa mnyama huyu hufikia mita 28 mpaka mita 33, ambapo majike huwa warefu zaidi ya madume na kwa uzito nyangumi hufikia mpaka tani 200, wakati watoto huwa na uzito wa tani tatu mpaka tano na urefu wa mita saba, Nyangumi hupumua kwa kutumia pua ambazo ni matundu mawili yaliyopo katika kichwa chake, mkia wake mwishoni hujigawa na kuwa na uelekea wa pande mbili yaani kushoto na kulia, nyangumi hula zaidi ya tani tatu kwa siku na mawindo yake hufuata chini ya maji ambapo kuna makundi makubwa ya dagaa.
 
Pamoja na kuishi baharini na katika kina kirefu maajabu ya nyangumi ni kwamba huwa hawazami chini sana katika maji, na yote hiyo ni kwa sababu hutumia mapafu katika mfumo wake wa upumuaji, hivyo akienda umbali mrefu sana hufika mita 300, na kutokana na aina ya upumuaji wake, mnyama huyu ni miongoni mwa wanyama ambao hulala kwa machale machale kwa kuhofia kifo majini, hutumia muda mfupi sana kulala na wakati wote mwili wake anapolala huwa na muonekano wa kusimama wima huku upande mmoja wa ubongo ukibaki unafanya kazi kama kawaida kwa madhumuni makubwa ya kujirinda na kifo.
 
Nyangumi pamoja na kuwa na umbo kubwa lakini ndani ya maji huwa na kasi kubwa, ana uwezo wa kukimbia km 50 kwa saa moja, na mbio hizo ndio humsaidia kukamata windo lake kwani hufanya mashambulizi ya kushitukiza, kiasi cha kufanya dagaa kushituka wakati tayari wamekamatwa, Sauti ya viumbe hawa ni nzito sana majini na wanapounguruma viumbe wengine hutetema na kutulia, kwani ndiye kiumbe pekee ambaye huweza kurusha sauti yake kwa umbali mkubwa sana, unapopita katika ukanda wao huonekana kwa urahisi kwa staili yao ya upumuaji kwa kurusha maji juu na namna wanavyoogelea kwa kuipinda miili yao ambayo hujitokeza juu na wakati mwingine wakiitupa miili yao juu ya maji na kuzama tena.
 
9. Nyangumi ni mnyama asiyekunywa maji ya kabisa, hii ni kwa sababu huishi baharini ambako hupatikana maji chumvi ambayo si rafiki kwake, hivyo kiu chake hukatika kwa jinsi chakula alichokula kitakavyokuwa kinachakatwa na kufyonzwa majimaji.
 
13. Kwa asili viumbe hawa huishi kwa mitala, Nyangumi dume humiliki majike wengi na hawana matatizo kwakuwa hufahamu madume ni wachache, hivyo jike mmoja anaposhika mimba huwapa nafasi majike wenzie kufurahi na dume wake.
 
Back
Top Bottom