Kiboko ni Mnyama ambaye maisha yake amewekeza katika makazi ya aina mbili, huishi nchi kavu pamoja na majini, anatambulika kama farsi wa majini, kwa ufanano ukimtizama vyema huonekana kama nguruwe, ila kwa taarifa yako huyu ni miongoni ya wanyama ambao huishi majini kama ilivyo kwa nyangumi na pomboo, ukimtoa tembo na faru, kiboko ndio mnyama mkubwa kwa wanyama wa ardhini, ni mnyama mtata, mkorofi na mbishi vilivyo, ukimzidi nguvu nchi kavu atakimbilia majini, lakini kwa binadamu kumshinda nguvu si jambo jepesi hata kidogo, ndiyo mnyama mkubwa wa ardhini ambaye ameua binadamu wengi kuliko mnyama yoyote mkubwa kama simba, chui nk.