22. Kwa ukubwa wake Nyangumi binadamu wameweza kutengeneza hata hadithi ya kwamba anaweza kutengeneza kisiwa na binadamu wakafanya shughuli zao juu ya mgongo wake mpaka hapo atakapoondoka, ifahamike hadithi hiyo haina ukweli kuhusiana na maisha ya mnyama huyu, ni utunzi wa kufikirika tuu.
Pengine utakuwa umeshajiuliza ya kwamba sasa kama Nyangumi na sifa hizo zilizoainishwa inakuwaje pindi vinapopita vyombo vya usafiri kama meli, boti nk, au unaweza jiuliza je Nyangumi hula watu ! Au ukataka kujua kama ni mkorofi au lah !