Tofauti na samaki ambao huendeleza vizazi vyao kwa kutaga, nyangumi si samaki bali ni mnyama anayeishi baharini, ingawa umbo lake hufanana na samaki mkubwa hususani kichwa, baadhi ya sehemu za mwili na mkia, lakini hayo hayaondoi sifa yake ya kuitwa mnyama kwani ni kiumbe anayezaa na kunyonyesha, jike huwa na matiti mawili ambayo humsaidia kumpatia ndama wake chakula kwa kumnyonyesha, hubeba mimba kwa miezi 12 na huzaa mtoto mmoja tuu, ambapo anapozaliwa hutanguliza mkia ili kuzuia kifo kinachoweza tokana na kukosa hewa, na punde baada ya kuzaliwa tuu mtoto huyo huanza kuogelea kuelekea juu ya uso wa bahari kwa msaada wa mama yake ili akapate hewa, ndama wa nyangumi hunyonya takribani lita 250 mpaka 400 za maziwa kutoka kwa mama yake kila siku, mpaka hapo atapotimiza mwaka mmoja.