Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wasukuma watano walienda baa ila kwa bahati mbaya wakawa hawajui majina ya bia wanazozihitaji. Baadae wakaingia Wachaga watatu wakaagiza Kilimanjaro sita… Mda uleule akaja mkurya akaagiza Serengeti mbili… Hawajakaa sawa akaingia Muhaya akaagiza Balimi saba Wasukuma wakasema aanhaaaa… kumbe kila mtu anakunywa bia za kwaooo… Wakaanza; (kwa lafudhi ya kisukuma kwa kukundamiza) "… Wee limhudumu… Mhudumu; sema nawasikiliza mabosi. Wasukuma; (kwa kukandamiza) Leta-NYEHUNGE mbili USHILOMBO tatu, SHINYANGA nne, BHARIADI tano, na GEITA saba… !!! Mhudumu: (kwa hasira) "JASHIRAGAA….!!!" 😂😂😂😂😂😂
 
Viatu hivi vinapatikana Masaki Peninsula mane lavusi mi walahi [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]...

Nakereketwa kuwa kwenye iginoa listi sijui. Ngoja nilog off nipumzike vinginevyo kuna hatari ya kujikuta kwenye iginoa list hata tatu leo aisee...[emoji2221][emoji2221][emoji2221][emoji2221][emoji85]
 
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] carbamazepine
 
STRAIKA, Sergio Aguero amewasha moto kwenye Ligi Kuu England na sasa amebakiza hat-trick moja tu kufikiria rekodi iliyodumu kwa miaka kibao iliyowekwa na Alan Shearer.
 
Aguero alifunga mara tatu kwenye mechi dhidi ya Arsenal uwanjani Etihad na jambo hilo limemfanya awe amefikisha hat-trick 10 kwenye Ligi Kuu England. Hii hapa orodha ya mastaa baadhi ambao wamefunga hat-trick kibao kwenye Ligi Kuu England.
 
Robin van Persie – Hat-trick 5

Straika wa Kidachi, Robin van Persie kwenye Ligi Kuu England alitamba akiwa na vikosi vya Arsenal na Manchester United. Hakika kiwango chake kilimfanya kuwa mmoja wa washambuliaji moto waliowahi kutokea katika ligi hiyo huku akiwa na rekodi ya kufunga hat-trick tano. Hat-trick yake ya mwisho alifunga Aprili 22, 2013 na kuisaidia Manchester United kunyakua ubingwa wao wa 20 wa Ligi Kuu England. Mchezaji mwingine aliyefunga hat-trick tano ni Andy Cole na Ian Wright.
 
Dimitar Berbatov – Hat-trick 5

Kwenye kikosi cha Manchester United kuliwahi kutokea huduma moto kabisa ya fundi wa mpira, Dimitar Berbatov. Lakini, supastaa huyo kabla hajatua Old Trafford alikuwa akifanya yake huko Tottenham Hotspur na Man United ilimsajili kwa pesa nyingi sana. Berbatov rekodi zake za mabao kwenye Ligi Kuu England zinaonyesha kwamba alifunga hat-trick mara tano tofauti, huku moja ya hat-trick zake ilikuwa kwenye mechi dhidi ya mahasimu wakubwa kabisa wa Man United, Liverpool. Staa mwingine wa Man United aliyepiga hat-trick tano ni Mdachi Ruud van Nistelrooy.
 
Luis Suarez – Hat-trick 6

Straika wa Uruguay, Luis Suarez kwa sasa anafanya mambo yake huko kwenye La Liga akiwa na kikosi cha Barcelona. Lakini, asikwambie mtu, mshambuliaji huyo alipokuwa Liverpool alikuwa tishio kwelikweli kwenye Ligi Kuu England. Suarez kwa sasa anatesa mabeki wa Hispania na pacha wake Lionel Messi, lakini huko alikoondoka kwenye Ligi Kuu England ameacha kumbukumbu nzuri ikiwamo ya kufunga mabao matatu matatu kwenye mechi moja mara sita tofauti. Suarez ana hat-trick sita kwenye Ligi Kuu England huku mara yake ya mwisho kuweka kwenye kamba mabao matatu katika mechi moja ilikuwa Machi 22, 2014 ambapo Liverpool ilikaribia kabisa kubeba ubingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…