Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wayne Rooney – Hat-trick 7

Supastaa, Wayne Rooney kwa sasa jina lake limeweka heshima kubwa huko Manchester United na kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England. Fowadi huyo ndiye kinara wa mabao kwa timu hizo mbili, akiongoza kwa mabao Man United na akiweka rekodi hiyo kwenye kikosi cha England pia. Kwa sasa fowadi huyo aliyetamba kwenye Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Everton na Man United anacheza soka lake huko Marekani. Rekodi zake kwenye Ligi Kuu England, Rooney amefunga hat-trick saba na hivyo kuwa kwenye orodha ya wakali waliotupia mara nyingi tofauti mabao matatu matatu kwenye mechi za ligi. Hat-trick yake ya mwisho kwenye ligi hiyo, Rooney alifunga Novemba 29, 2017 akiwa kwenye kikosi cha Everton.
 
Harry Kane – Hat-trick 8

Straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane kwa sasa yupo nje ya uwanja na kushindwa kuitumikia timu yake kutokana na kuwa majeruhi. Jambo hilo limekuwa majanga makubwa kwa kocha Mauricio Pochettino kwa sababu kimsingi, Kane ndiye mshambuliaji wake moto anayemtegemea kwa kiasi kikubwa katika kufunga mabao. Kwenye Ligi Kuu England msimu huu, Kane ameshaweka wavuni mabao 14, lakini akiwa na rekodi ya kubeba Kiatu cha Dhahabu cha ligi hiyo mara mbili. Kane hakuishia hapo, ameonyesha uhodari wa kufunga pia bao tatu tatu kwenye mechi moja akifanya hivyo kwenye mechi nane tofauti. Lakini, kwa muda mrefu, Kane hajafunga hat-trick, ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Boxing Day, 2017.
 
Thierry Henry – Hat-trick 8

Gwiji wa Arsenal, Thierry Henry hivi karibuni alipambana vichwa vya habari kwenye magazeti kutokana na kufutwa kazi ya ukocha kwenye kikosi cha AS Monaco baada ya kudumu na timu hiyo kwa miezi minne tu. Kabla ya kubamba kibarua hicho, Henry alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji akifanya kazi chini ya kocha Roberto Martinez. Sawa, pengine Henry ameshindwa kutamba kwenye benchi akiwa kocha, lakini alipokuwa mchezaji shughuli yake ilikuwa pevu uwanjani, ukipata mabeki waliowahi kukabiliana naye, watakuhadithia vizuri. Henry anashikilia rekodi ya kuwa kinara wa mabao huko England, lakini akiacha kumbukumbu pia ya kufunga hat-trick nyingi kwenye Ligi Kuu England akifanya hivyo mara nane, huku hat-trick yake ya mwisho alifunga Mei 7, 2006.
 
Michael Owen – Hat-trick 8

Kwenye Ligi Kuu England, fowadi moto kabisa Mwingereza Michael Owen alitamba kwenye vikosi vya Liverpool, Manchester United, Newcastle United na Stoke City. Liverpool ndio iliyofaidi kiwango bora kabisa cha mshambuliaji huyo kabla ya kutibuliwa na majeruhi ya mara kwa mara, akienda zake Real Madrid kabla ya kurudi England kwanza kujiunga na Newcastle United kabla ya kuibukia huko Old Trafford na kisha baadaye kwenda kumalizika mpira wake kwenye kikosi cha Stoke City. Ubora wa Owen kwenye Ligi Kuu England hauna mashaka na ndio maana amekuwa mmoja wa wakali waliopiga hat-trick nyingi kwenye ligi hiyo, akitupia kwenye nyavu hat-trick nane, huku mara yake ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Desemba 17, 2005.
 
Robbie Fowler – Hat-trick 9

Huko Anfield, mashabiki wa Liverpool walimwita Robbie Fowler kuwa ni mungu wao. Kuna baadhi ya wachambuzi wanaamini pengine hiyo ndiyo laana inayoifanya timu hiyo hadi sasa kushindwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England licha ya kukaribia kufanya hivyo zaidi ya mara mbili. Msimu huu wanaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa, lakini kama watashindwa basi itabidi waende kutubu kutokana na kumwona Fowler kama mungu wao. Kilichowafanya Kop pengine kumfanya Fowler awe wanavyofikiria wao ni ule uwezo wake wa kufunga mabao, ambapo rekodi zinaonyesha kwamba staa huyo amefunga hat-trick tisa kwenye Ligi Kuu England. Hat-trick yake ya mwisho Fowler alifunga Boxing Day, 2001.
 
Sergio Aguero – Hat-trick 10

Jina la Sergio Aguero bila shaka litakuwa linaleta hasira kubwa sana kwa mashabiki wa Arsenal kutokana na kile alichowafanya juzi Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Fowadi huyo Muargentina kwenye mechi hiyo alifunga hat-trick kuisaidia Manchester City kushinda 3-1 na hivyo kuwasogelea Liverpool kwenye mbio za ubingwa ambao usiku wa jana Jumatano walikuwa na kibarua kizito cha kuwakabili West Ham United kwenye uwanja wao huko London. Mabao yake hayo matatu aliyofunga Aguero kwenye mechi hiyo yamemfanya kuweka rekodi yake moto ya kufunga hat-trick 10 tangu alipotua kwenye ligi na sasa amebakiza moja tu kufikia rekodi ya kinara wa hat-trick, Alan Shearer. Aguero bado yupo kwenye ligi na kwa sababu kufunga halijawahi kuwa jambo gumu kwake, basi huenda akavunja rekodi hiyo kabla ya msimu huu kumalizika.
 
Alan Shearer – Hat-trick 11

Supastaa, Alan Shearer hakutaka kabisa kwenda kujiunga na klabu kubwa kwenye Ligi Kuu England kwani aliwakatalia Manchester United wakati walipohitaji huduma yake. Pengine Shearer hakuona umuhimu wa kufanya hivyo ikiwa kama ubingwa ilikuwa tayari ameshaubeba akiwa na kikosi cha Blackburn Rovers. Shearer alitamba na timu hiyo kabla ya kwenda kuwasha moto kwenye kikosi cha Newcastle United na hivyo kufanikiwa kuwa gwiji katika timu hizo mbili, hasa kutokana na uwezo wake wa kupasia mipira nyavuni. Shearer ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao kwenye Ligi Kuu England, huku akishikilia pia rekodi ya kufunga hat-trick nyingi zaidi kwenye historia ya ligi hiyo akifanya hivyo mara 11. Hat-trick yake ya mwisho Shearer kufunga ilikuwa Septemba 19, 1999.
 
Mastaa waliopiga hat-trick 4

Kwenye orodha hiyo ya wakali wa Hat-trick kwenye Ligi Kuu England wale waliofanya hivyo mara nne wapo wengi, ikiwamo Fernando Torres, Jermain Defoe, Carlos Tevez, Dwight Yorke, Teddy Sheringham, Jimmy Floyd Hasselbaink, Les Ferdinand, Yakubu kwa kuwataja kwa uchache, huku wenye tatu wamo Didier Drogba, Nicolas Anelka, Emmanuel Adebayor, Romelu Lukaku, Ole Gunnar Solskjaer na wakali wengine kibao.
 
KUNA sehemu za kumdhamini kocha Unai Emery, lakini si kwa Pep Guardiola.

Kwa kifupi tu, usithubutu kumwekea dhamana ama ukaweka mkeka wako kwa Emery anapokuwa na mechi dhidi ya Guardiola. Kama utabeti hapo kwamba Emery atashinda, basi mkeka wako utachanika asubuhi tu na kumtajirisha mhindi.
 
Juzi Jumapili, Arsenal ilikwenda kumenyana na Manchester City kwenye Ligi Kuu England. Sawa, mechi hiyo yenyewe tu ilikuwa ikijieleza kwamba mara nne walizokutana kabla ya mechi hiyo, Man City zote alishinda.
 
Wakati mashabiki wa Arsenal wakiwa na matumaini kwamba, ingekuwa zamu yao kushinda kwenye mechi hiyo ya Jumapili, walisahau kuwa kwenye benchi lao yupo Emery, ambaye hajawahi kushinda mechi yoyote aliyocheza dhidi ya timu ya Guardiola. Yaani kila akiingia ni maumivu.
 
Ubao wa rekodi unavyosoma kwa sasa ni aibu. Katika mechi 12, Emery alipokabiliana na Mhispaniola mwenzake huyo, ameshinda SIFURI, sare nne na amekumbana na vichapo mara nane.
 
Rekodi zao za kukutana zilianzia huko Hispania, wakati Emery alipokuwa kocha wa Valencia na Guardiola akiwa Barcelona. Kwenye Ligi Kuu England wamekutana mara mbili, mechi zote Emery kachapwa. Katika mechi hizo mbili za kwenye ligi, Emery amewahi kukutana na kipigo cha aibu cha mabao 5-1.
 
Kwa ujumla wa mechi zote 12 walizokutana, timu ya Emery imefunga mabao nane tu, wakati Guardiola timu yake imefunga mabao 27. Kwa hesabu hizo, Emery ana deni la mabao 19 kwenye mechi alizokabiliana na Guardiola.
 
Kipigo kizito zaidi Emery alichowahi kukutana nacho kutoka kwa Guardiola ni kile cha 5-1 katika msimu wa 2011/12 huko kwenye La Liga, licha ya kuwa kabla ya hapo, Emery aliwahi kuchapwa 4-0 na Guardiola katika msimu wa 2008/09 na mabao 3-0 katika msimu wa 2009/10.
 
Ukiweka kando Emery kwamba hamwezi Guardiola, kwa upande wa Arsenal wao kwa ujumla wanashindwa kumkabili kabisa straika matata wa Argentina, Sergio Aguero, ambaye ameigeuza beki ya Arsenal kuwa uchochoro na kufunga kwa kadri anavyotaka.
 
Ile hat-trick ya juzi Jumapili imemwongezea tu idadi ya mabao yake aliyofunga dhidi ya timu huyo, ambapo ameshawafunga mabao manane kwenye mechi 13 za Ligi Kuu England. Hii ni ishara kwamba, Emry anapaswa kurudi darasani kujifunza namna ya kukabiliana na Guardiola, ambaye kwa sasa amezidi kuwa moto kutokana na kikolsi chake kusheheni mastaa wakubwa.
 
.GWIJI wa Barcelona, Hristo Stoichkov amedaiwa kumwaandikia barua supastaa wa Kibrazili, Philippe Coutinho.
 
Staa huyo wa zamani wa Liverpool, Coutinho kwa sasa kiwango chake kimeporomoka na kumekuwa na ripoti huenda akaachana na maisha ya Barcelona itakapofika mwisho wa msimu huu, dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…