Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Timu ya Liverpool imejikuta kwenye presha ndani ya kikosi hicho baada ya kutoka sare ya pili ya bao 1-1 dhidi ya West Ham kwenye mchezo wa Ligi Kuu England jana Jumatatu usiku.
 
Liverpool ilijikuta ikitoka sare dhidi ya West Ham huku wasiwasi wao ukiwa kwa wapinzani wao wa karibu Manchester City ambao wanaweza kupanda kileleni iwapo watashinda mchezo wao dhidi ya Everton utakaopigwa Jumatano usiku.
 
Katika mchezo huo wa jana makocha wa timu zote, walijikuta wakimvaa mwamuzi wa mchezo huo lakini yote ni katika presha ya kupata alama tatu muhimu.
 
Hivyo, Liverpool wameendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya tofauti tatu, huku wakiwa na mchezo mwingine wikiendi hii watakapokutana na Bournemouth.
 
Klopp amesema kwamba amesema kwamba bado wapo kwenye mbio za ubingwa huku akisisitiza bahati ilikuwa upande wa West Ham jambo lililowafanya kugawana alama moja moja.
 
Alisema haikuwa matarajio yake, hata hivyo upande mwingine maandalizi ya kikosi chake yaliingiwa dosari kutokana na kuwapo majeruhi kama Jordan Henderson na Gino Wijnaldum. Pia James Milne alikuwa mgonjwa. Hivyo ugumu ulijitokeza kutokana na mazingira hayo pamoja na nafasi ubra ya wapinzania wao.
 
Naye Kocha wa West Ham, Manuel Pellegrini alisema kila mchezo huwa ni mgumu haijalishi walicheza na vinara wa Ligi Kuu au timu yenye safu imaraya ulinzi.
 
Alisema jambo linalomhuzunisha ni kwamba walitengeneza nafasi nne za mabao lakini hawakuzitumia ipasavyo.
 
Nyota wa PSG, Neymar ambaye mchezaji ghari duniani leo Jumanne tarehe 05 Februari anatimiza umri wa miaka 27, huku nyota huyo akiwa nje ya uwanja kutokana na kuuguza majeraha.
 
Neymar bado anauguza majeraha aliyoyapata katika mechi yao ya Kombe la Ufaransa wiki iliyopita. Neymar alisherehekea siku yake ya kuzaliwa jana Jumatatu asubuhi jijini Paris Ufaransa akiwa ametinga mavazi yenye rangi nyekundi pamoja na wapambe wake.
 
Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na wachezaji wanzake wa PSG na mastaa mbalimbali maarufu duniani.
 
OLE Gunnar Solskjaer anachanua. Juzi Jumapili alishinda mechi ya saba ya Ligi dhidi ya Leicester City na kuiweka Manchester United katika nafasi ya tano mbele ya Arsenal. Hata hivyo, mtu mmoja anadai kwamba suala la kupewa ukocha wa kudumu bado kidogo.
 
Gary Neville, staa wa zamani wa Manchester United ambaye alicheza pamoja kwa mafanikio na Solskjaer Old Trafford anaamini kwamba, kocha huyu wa muda anahitaji kushinda baadhi ya mechi za kiume kwa ajili ya kupewa nafasi hiyo jumla.
 
Neville anadai kuna mechi chache za kibabe zinakuja usoni mwa Solskjaer na zitampima vilivyo kama ataweza kuhimili mikiki endapo atapewa nafasi ya kuwa kocha wa kudumu wa Manchester United, baada ya kung’ara katika ukocha wa muda tangu alipopewa timu Desemba, mwaka jana baada ya kutimuliwa kwa Jose Mourinho (Special One).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…