Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabu Ley, Luambo Luanzo Makiadi and Verkys Kiamuangana.
Kinshasa 1986
FB_IMG_1549532087754.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
*UNATAKA KUWA NA AMANI MWANA UZI?

*_Kama unataka kuwa na amani zingatia haya:-_*

1. _Futa uadui na yeyote hata kama alikukosea namna gani, kisha dharau na kaa kimya utaona moyo wako unakuwa huru._

2. _Sema kinachokukwaza bila kuhofu unayemwambia na usiache neno liote kutu rohoni._

3. _Achana na visasi, vinyongo na chuki zisizo na faida, kwani hayo yanakuathiri wewe mwenyewe._

4. _Jiepushe na habari za watu hata ukisikia jambo liache hapo hapo, akili yako irudi kwenye mambo yako, kwani kupenda habari za watu zitakufanya ukose muda wa kushughulikia masuala yanayokuhusu na mwisho wa siku zitakukosesha amani._

5. _Usijipendekeze kwa mtu kwa ajili ya kitu. Jipe thamani japo huna kitu, watu watakuheshimu._

6. _Acha kutoa siri zako kumwambia mtu hata awe rafiki yako namna gani. Unayemshirikisha siri, siku mkigombana siri zako zitageuka kuwa silaha dhidi yako na kukunyima amani._

7. _Siku zote pigania furaha yako, usiache mtu akupokonye. Kwa sababu ukikosa furaha hutakuwa na amani._

8. _Jitahidi kusamehe kabla aliyekukosea hajakuomba msamaha. Kufanya hivyo kutakuacha huru na utumwa wa vinyongo._

9. _Ondoa dhana mbaya kwa watu wanaokuzunguka hata kama umesikia wanakusema, wapotezee kama hujasikia; utawaumiza sana kuliko ungewauliza. Siku zote kimya ni jibu la mpumbavu._

10. _Hakuna kitu kinachorudisha maendeleo ya watu kama vinyongo na kutosamehe, kwani utapoteza muda mwingi kumfikiria aliyekukosea kuliiko kufikiria maisha yako._
_Ukifuata muongozo huu utanenepa bila kula vinono na mapochopocho._

_Utanawiri bila pesa mfukoni na dunia utaishi kwa amani na kujiona umebarikiwa.


Good morning!!!!!!!!![emoji173]
Sent using Jamii Forums mobile app
Ngumu sana hii. Bado nina kinyongo kikali balaa
 
Hahahahaahha!!!
Jaribu kukiondoa, kitausinyaisha moyo wako bure..

Halafu siku zote nakuona sio mtu wa vinyongo eti, maana unampa mtu makavu pale pale, hupepesi....Unaachilia ya moyoni maisha yanaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kesi niliyonayo bado sijampa mtu makavu ndo maana kinyongo hakiishi.
This time ngoja nijaribu kupotezea kwa maslah ya moyo. Mwaga pointi nyingine tunajifunzapo hapa
 
Back
Top Bottom