Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, yupo katika mazungumzo ya kina kuhusu kuimarisha mkataba wake ambao huenda ikachangia kuongezwa kwa mshahara wake kwa zaidi ya mara mbili na mkubaliano ya thamani ya £200,000 kwa wiki katika mkataba wa muda mrefu(Star)
Huenda Paris St-Germain ikatafuta kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 27, katika msimu w a joto. (Le10 Sport, kupitia Sun)
Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United, Jose Mourinho anatarajiwa kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa Inter, Beppe Marotta kuhusu kuchukua usukani katika klabu hiyo ya Italia kwa mara ya pili. (Mirror)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Philippe Coutinho inaarifiwa 'amehuzunishwa' kuwepo Barcelona, lakini anaendelea kupata usaidizi kutoka kwa wachezaji wenzake na meneja wake. Manchester United na Chelsea zinafikiria kumfukuzia mchezjai huyo wa miaka 26 katika msimu wa joto. (Sport, kupitia Metro)
Arsenal inaongoza katika kumfukuzia mlinzi wa Benfica Alex Grimaldo, mwenye umri wa miaka 23. Manchester City, Napoli na Inter Milan zote zimehusishwa na beki huyo wa kushoto. (Mundo Deportivo, kupitia Express)
Mchezaji aliyelengwa na Chelsea, Daniele Rugani, mwenye umri wa miaka 24 mchezaji wa timu ya taifa ya Italia anatarajiwa kupokea mkataba ulioimarika huko Juventus hadi 2023. (Calciomercato)
Manchester United bado ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Napoli, Kalidou Koulibaly, mwenye umri wa miaka 27, Milan Skriniar, mwenye umri wa miaka 23, wa Inter na pia ina hamu ya kumsajili mlinzi wa tatu, Joachim Andersen, mwenye miaka 22 wa Sampdoria. (Manchester Evening News)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.