Timu nyingine
Kwenye kikosi cha Watford, mchezaji wao wa mwisho kufunga hat-trick kwenye ligi alikuwa, Mark Falco na hiyo ilikuwa miaka 35 iliyopita huko, wakati alipofunga tatu kwenye mechi dhidi ya Aston Villa iliyofanyika Oktoba 1986. West Ham United wao rekodi zao zinaonyesha kwamba mchezaji wao wa mwisho kuwafungia hat-trick kwenye ligi alikuwa Andy Carroll, ambaye alifanya hivyo kwenye mechi ya sare ya 3-3 dhidi ya Arsenal, Aprili 2016.