Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sarri alishudia kikosi chake kikipokea kipigo cha mabao 6-0 kutoka Manchester City, jambo lililofanya watabidili wa michezo kubashiri kuwa ndiye kocha anayefuata kutimuliwa England, huku Zidane akipewa nafasi kubwa ya kuchukua jukumu hilo pamoja na Gianfranco Zola.
 
Kipigo cha Chelsea kutoka kwa City kimewaporomosha hadi nafasi ya sita jambo lililofanya gazeti la The Sun kudai kuwa siku zake zinahesabika ndani ya Stamford Bridge.
 
Siyo tu mashabiki wa Chelsea na wajumbe wa bodi wanaopata tabu kwa sasa. Hatma ya nyota wao Eden Hazard ipo shakani kwa sababu Mbelgiji huyo amebakiza miezi 18 katika mkabata wake na inavyoonekana anataka kutimkia Real.
 
Lakini Hazard ni shabiki mkubwa wa Zidane na inavyooneka ujio wa Mfaransa huyo itakuwa ni sababu kubwa kwake kubaki London.
 
Hazard amekuwa Chelsea tangu alipojiunga nao akitokea Lille mwaka 2012. Amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu, pia akichukua mara moja Kombe FA, Kombe la Ligi na Europa Ligi.
 
Back
Top Bottom